Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya (katikati) akizungumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani yaliyofanyika leo Juni 7, 2023 katika Ofisi za makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
****************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
WADAU mbalimbali wametakiwa kushiriki kikamilifu katika mikakati mbalimbali yenye lengo la kuzuia, kugundua na kujenga uwezo katika kukabiliana na vihatarishi vinavyoweza kusababisha uchafuzi wa chakula, na hivyo, kuathiri usalama wake.
Wito huo umetolewa leo Juni 7,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani ambayo hufanyika Juni 7 kila mwaka.
Amesema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), inakadiriwa kuwa kila mwaka mtu mmoja katika kila watu kumi hupata madhara yatokanayo na ulaji wa chakula kisicho salama duniani, na kuwa, watu 420,000 kati ya wanaougua hufariki.
"Imeelezwa pia kuwa, madhara ya magonjwa yatokanayo na chakula kisicho salama ni makubwa zaidi katika nchi zinazoendelea, na wahanga zaidi wakiwa ni watoto walio chini ya miaka mitano". Amesema Dkt.Ngenya.
Aidha amesema kuwa Ili kuhakikisha upatikanaji wa chakula salama na bora, uandaaji wa viwango vya chakula huzingatia mifumo bora ya uzalishaji wa chakula husika, ikiwa ni pamoja na mfumo bora wa kilimo, mfumo bora wa usindikaji na mfumo wa uzingatiaji wa kanuni bora za usafi.
Ameeleza kuwa viwango vya bidhaa za chakula huandaliwa ili pamoja na matakwa ya kibiashara, kuhakikisha kuwa chakula kinachomfikia mlaji ni salama. Viwango hivyo ni mahususi kwa ajili ya kumuongoza mzalishaji kuzalisha bidhaa bora na salama kwa mlaji na zinazokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
"Kutokana na umuhimu wake katika kulinda afya ya jamii, viwango vya chakula ni viwango vya lazima (mandatory standards), hivyo kila mdau katika mnyororo wa chakula hana budi kuvizingatia ili kuhakikisha kuwa chakula ni salama kwa mlaji". Amesema
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akizungumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani yaliyofanyika leo Juni 7, 2023 katika Ofisi za makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Udhibiti Ubora TBS, Bi. Gwantwa Mwakipesile akizungumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani yaliyofanyika leo Juni 7, 2023 katika Ofisi za makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wakishiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani yaliyofanyika leo Juni 7, 2023 katika Ofisi za makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau walioshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani yaliyofanyika leo Juni 7, 2023 katika Ofisi za makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa TBS katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani yaliyofanyika leo Juni 7, 2023 katika Ofisi za makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
Social Plugin