NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Yanga imeshindwa kuwa mabingwa licha kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa Fainali kombe la Shirikisho mkondo wa pili mara baada ya matokeo ya kwanza akiwa nyumbani kuruhusu kufungwa mabao 2-1.
Mchezo huo ulijaa vitimbwi mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa USM Algers hasa kuwasha mafataki na kusababisha moshi mwingi kujaa uwanjani na kufanya mpira kusimama mara kadhaa kwenye mchezo huo.
Yanga Sc ilianza kupata bao kupitia kwa beki wao Djuma Shabaan kwa mkwaju wa penati dakika za mwanzo kipindi cha kwanza, bao ambalo liliweza kudumu mpaka dakika 90 ya mchezo.
Fiston Kalala Mayele amefanikiwa kuchukua kiatu cha ufungaji bora kwenye michuano hiyo kwa kufanikiwa kuwa kinara wa upachikaji wa mabao baada ya kupachika mabao 7 kwenye michuano hiyo ambayo imefikia tamati leo.
Social Plugin