Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga akitoa hotuba ya kufungua taftishi hiyo leo Tar.8/6/2023, Lindi.
Mwakilishi wa Baraza la Ushauri la Serikali (GCC) Conrad Milinga,akitoa maoni yake wakati wa taftishi hiyo.
Meneja wa EWURA, Kanda ya Mashariki, Mha. Nyirabu Musira, akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano huo.
Na.Mwandishi Wetu
Wananchi wanaohudumiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Lindi (LUWASA), leo 6 Juni 2023, wametoa maoni yao juu ya maombi ya ya kurekebisha bei za majisafi na usafi wa mazingira, wakati w mkutano wa taftishi ulioandaliwa na EWURA.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga, wakati akifungua mkutano huo, amewataka wananchi kutoa maoni yao kizalendo, ili wapate bei zinazoendana na huduma bora za maji.
Kaimu Mkurugenzi wa LUWASA Bi. Zamda Keya ameeleza sababu kuomba marekebisho ya bei hizo ni pamoja na kuwezesha mamlaka kumudu gharama za umeme kwa asilimia mia, kusogeza mtandao karibu kwa wananchi, kuongeza upatikanaji wa huduma kufikia 95%, na kumudu eneo la huduma lililo ongezeka la jimbo la Mchinga.
Akitoa neno la utangulizi, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, ambaye ni Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Mha. Nyirabu Musira alisema, mkutano huo ni sehemu ya uchunguzi unaofanywa na EWURA, kupata maoni ya wadau kabla ya kutoa uamuzi kuhusu bei za maji.
Ukusanyaji wa maoni umejumuisha wananchi wa manispaa ya Lindi, Baraza la Ushauri la Serikali la Huduma zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA GCC) na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC).
Social Plugin