Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA ELIMU, BENKI YA NBC WAZINDUA MPANGO WA UFADHILI WA MASOMO YA UFUNDI STADI KWA VIJANA KUPITIA VETA

Waziri Elimu, Sayansi na Taknolojia Prof.Adolf Mkenda akipokea mfano wa hundi ya shilingi Milioni mia moja (100,000,000/=) kwaajili ya ufadhili wa masomo kwa vijana wa VETA wakati wa uzinduzi wa mpango rasmi wa ufadhili wa masomo ya ufundi stadi kwa vijana, kupitia Mamlaka za Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini yaani VETA.Hafla hiyo imefanyika leo Juni 9,2023 Jijini Dar es Salaam.

****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SAAAM

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Benki ya NBC wamezindua mpango rasmi wa ufadhili wa masomo ya ufundi stadi kwa vijana, kupitia Mamlaka za Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini yaani VETA.

Mpango huu maalum ujulikanao kama “NBC Wajibika Scholarships” utalenga kutoa ufadhili kwa wanafunzi 1,000 katika vituo mbalimbali vya VETA hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Juni 9,2023 Jijini Dar es Salaam, Waziri Elimu, Sayansi na Taknolojia Prof.Adolf Mkenda ameipongeza Benki ya NBC kwa hatua ambayo wameifanya hasa kuhakikisha vijana ambao watapata fursa ya ufadhili huo watawapa nafasi ya kujifunza masuala ya fedha hasa kwenye masuala ya ujasiriamali na kuweza kujitegemea.

Amesema kuna umuhimu mkubwa Vyuo vyote vya Ufundi na Vyuo vya Amali nchini vikasaidia kupata idadi kubwa ya watu wenye uwezo wa kuzalisha vitu kama nguo, viatu na vitu vingine ambavyo vitasaidia kuongeza ajira hapa nchini kulinda fedha zetu za kigeni.

Aidha ametoa wito kwa wadau wengine waweze kujitokeza na kuungana na Wizara katika kuhakikisha vijana wengi wanaojiunga na VETA waweze kupata ufadhiri wa masomo

Amesema Serikali inaangalia namna ya kuboresha mafunzo katika VETA ili kuhakikisha vijana wanaohitimu wanakuwa na ujuzi mkubwa ambao utapelekea kujiajiri ama kuajiriwa kwa haraka zaidi kupitia mafunzo ambayo wamesomea.

Pamoja na hayo amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa VETA kwa ngazi za Wilaya nchini ambapo mpaka sasa wanaendelea naujenzi wa VETA 64 kwa mkupuo nchi nzima na mpaka sasa Mkoa mmoja ndo umebaki hauna VETA ya Mkoa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw.Theobald Sabi amesema Benki ya NBC imetenga kiasi cha shilingi milioni mia moja kushamirisha ufadhili huo. Masomo mbalimbali ya ufundi ikiwemo ushonaji, userelema, ufundi magari, ujenzi, Upambaji na mengineyo, yanufaika na mpango huu maalum.

Amesema zaidi ya ufadhili wa masomo, Benki pia itawaingiza vijana hao 1,000 katika mpango maalum wa elimu ya fedha ujulikanao kama “NBC Business Club” na kuwafungulia akaunti maalum za “NBC-KUA Nasi” zitakazowapa wasaa wa kutunza fedha bila gharama, kupata ushauri juu ya uwekezaji na kuwapa fursa za uwezeshaji kiuchumi kupitia mikopo ya kujiendeleza kibiashara.

"Benki ya NBC inaendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwa mdau mkubwa wa elimu na uwezeshaji kwa vijana kwani katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, imewekeza zaidi ya shilingi 350 milioni katika kutoa ufadhili wa masomo kwa vijana 70 katika Vyuo mbalimbali vya elimu ya juu nchini". Amesema

Makubaliano rasmi pamoja na kusaini makubaliano hayo yatafanyika Juni 28 kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia pamoja na Benki ya NBC ambao watakabidhi fedha kwaajili ya kutoa ufadhili.

Waziri Elimu, Sayansi na Taknolojia Prof.Adolf Mkenda akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango rasmi wa ufadhili wa masomo ya ufundi stadi kwa vijana, kupitia Mamlaka za Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini yaani VETA.Hafla hiyo imefanyika leo Juni 9,2023 Jijini Dar es Salaam
Waziri Elimu, Sayansi na Taknolojia Prof.Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango rasmi wa ufadhili wa masomo ya ufundi stadi kwa vijana, kupitia Mamlaka za Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini yaani VETA.Hafla hiyo imefanyika leo Juni 9,2023 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw.Theobald Sabi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango rasmi wa ufadhili wa masomo ya ufundi stadi kwa vijana, kupitia Mamlaka za Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini yaani VETA.Hafla hiyo imefanyika leo Juni 9,2023 Jijini Dar es Salaam


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com