Watu sita wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari dogo aina ya Toyota Hilux eneo la Shule ya Msingi Lumala wilayani Ilemela mkoani Mwanza walipokuwa wanafanya mazoezi pembezoni mwa barabara.
Ajali hiyo imetokea leo Jumamosi Juni 22, 2023 ambapo dereva huyo anayedaiwa kutokea nyuma yao alisababisha maafa hayo kisha kutokomea kusikojulikana.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema kikundi kinachoundwa na wafanyakazi wa Hoteli ya Adden Palace, wateja na majirani wa hoteli hiyo ndio waliopata ajali wakati wakifanya mazoezi.
Social Plugin