Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Veronika Peter (46) mkazi wa Zanzibar anadaiwa kujiua kwa kunywa sumu kisa kuelemewa na madeni mengi ya mkopo yaliyomshinda kulipa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Richard Mchonvu amesema hayo leo Julai 12, 2023 wakati akitoa taarifa ya matukio yaliyojiri ndani ya kipindi cha kuanzia Julai Mosi hadi leo.
“Veronika alikuwa akiishi Mpendae anadaiwa kujiua baada ya kuona ameelemewa na mzigo mkubwa wa madeni. Nitoe wito kwa akina mama tuache tamaa wengi wanakopa mikopo wananunua nguo nzuri huwezi kurudisha mkopo kwa nguo ulizozivaa mwilini,” amesema bila kufafanua alipokopa mkopo huo na kiasi alichokuwa anadaiwa.
Social Plugin