Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AVUNJIKA UUME AKIHONDOMOLA TENDO LA NDOA KWA KUKALIWA DODOMA


Picha haihusiani na habari hapa chini


Utafiti wa madaktari wa idara ya Magonjwa ya Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma umebainisha kuwa mitindo ya kujamiiana unaweza kusababisha uume uliosimama kwa muda mrefu kuvunjika.


Utafiti wa madaktari hao umechapishwa kwenye Jarida la kimataifa la case za Upasuaji (International Journal of Surgery Case Reports, 108(2023)108415) wameripoti kufanya upasuaji wa kuunga uume wa kijana mwenye umri wa miaka 27 uliyovunjika wakati akijamiana na mkewe.


Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti huo, ajali ya kuvunjika uume si suala lenye kujitokeza mara kwa mara, lina uwiano wa 1 kati ya watu 175,000.  


Hata hivyo, utafiti huo unadokeza kuwa, tafiti zilizofanyika katika mataifa ya Ulaya na Marekani zimeonesha kuwa asilimia 93.3 ya ajali za uume hutokana na kujamiiana, ambacho kilikuwa chanzo cha ajali ya Uume aliyopata kijana aliyetibiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.


Vile vile, ajali za kuvunjika uume kwa kujichua  zinashika nafasi ya piki kwa zikiwa na asilimia 10.


Mikao ya kujamiiana kama vile Mwanamke kukalia uume inatajwa kuwa chanzo kikuu cha ajali za kuvunjika uume. Imeeleza taarifa hiyo.

 Chanzo _ Uhondo Media

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com