Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi, Leo amehitimisha bonanza la michezo kwa maveterani wa timu mbalimbali lililofanyika wilayani Kishapu.
Bonanza hilo ambalo lililenga kuhitimisha sherehe za Sabasaba liliandaliwa na Maveterani wa wilaya ya Kishapu chini ya uongozi wa ndugu Sostenes na kufunguliwa hapo jana tarehe 08/07/2023 na mkuu wa wilaya ya Kishapu Mh. Modest Mkude.
Timu hizo za Maveterani zilizoshiriki ni pamoja na timu kutoka Shinyanga, Kakola, Kagongwa, Simiyu, Tabora, Musoma na timu mwenyeji ya Kishapu ambapo timu za Kishapu na Shinyanga zilifanikiwa kutinga fainali na Kishapu kufanikiwa kutwaa kombe.
Akiwa anakabidhi kikombe cha ushindi kwa mshindi wa Bonanza hilo, Kamanda MAGOMI alisema michezo ni afya, inaleta umoja na mshikamano.
Kamanda MAGOMI aliihimiza jamii ya wana Shinyanga kuipenda michezo ili kuleta mshikamano.
Bonanza hili pia lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wakiwemo Mbunge wa Kishapu Mh. Boniphace Butondo, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Mh. Lucy Mayenga pamoja na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Grace Bizulu.
Kamanda Magomi ameahidi kuendelea kuyatumia mabonanza na matamasha mbalimbali yenye kulenga kuleta mshikamano katika Jamii kwa lengo la kutokomeza uhalifu mkoani Shinyanga.
Social Plugin