Benki ya CRDB imetoa msaada wa madawati 100 katika shule ya Msingi Shunu Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Benki ya CRDB iitwayo 'KETI JIFUNZE' inayofanyika nchi nzima kwa kutoa msaada wa madawati kwa shule mbalimbali nchini zenye upungufu wa madawati.
Madawati hayo yamekabidhiwa Julai 21,2023 na Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana kwa Katibu Tawala wilaya Kahama, Hamad Mbega ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.
Social Plugin