Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo , leo tarehe 21 Julai, 2023 amefanya ziara ya kikazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kufanya kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya uwanja huo kwa lengo la kuimarisha mahusiano kati ya DCEA na JNIA.
Katika kikao hicho wamejadili na kubadilishana uzoefu wa kiutendaji na kuazimia mambo kadhaa yatakayosaidia kudhibiti usafirishaji na uingizaji wa dawa za kulevya nchini.
Social Plugin