Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI DKT. GWAJIMA AZINDUA JUKWAA LA BIASHARA LA WANAWAKE NA VIJANA SABASABA EXPO



Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati akifungua mkutano wa jukwaa la biashara la Wanawake na vijana katika Kijiji cha sabasaba Expo, lililoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na TANZAKWANZA.



Na WJJWM, DSM




Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amefungua mkutano wa jukwaa la biashara la Wanawake na vijana katika Kijiji cha sabasaba Expo, lililoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na TANZAKWANZA.

Waziri Dkt. Gwajima amewapongeza wote waliofika katika jukwaa hilo kwani ni dhahiri wameunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuendeleza sekta ya ujasiriamali kwa wanawake na vijana nchini.

“Hili ni jukwaa la kipekee linalotuwezesha kubadilishana mawazo, kushirikiana na kufikia suluhisho kwa lengo la kukuza sekta hii muhimu. Leo, tunashuhudia umuhimu mkubwa wa kuwawezesha wanawake na vijana katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo endelevu nchini Tanzania” amesema Dkt. Gwajima.

Aidha, Waziri Dkt.Gwajima amesema kuna haja ya kuwa na jukwaa moja la sekta zote ambazo zinagusa vijana, wanawake, biashara, benki na sekta nyingine muhimu katika kuinua biashara za wanawake na vijana.

Naye mwenyekiti Baraza la Biashara la Wanawake Tanazania (TWCC) Mercy E. Silla akizungumza kwa niaba ya wafanyabishara wanawake Tanzania ameshukuru waandaaji wa jukwaa hilo na kusema TWCC inaendelea kuwawezesha wanawake na kuboresha biashara za kila mwanamke.

“Tutaendelea kutangaza kwa wanawake ili waweze kuingia kwenye baishara na Mhe. Waziri unajua kuwa asilimia Hamsini nne (54) ya wafanyabishara wa kati na wadogo ni Wanawake hivyo kama TWCC tunajivunia . Kwa upande wa vijana tumeanza kuwekeza kwa vijana na si wakike tuu, hata na wa kiume kwahiyo tunaendelea na kuwawezesha vijana pia”. Amesema Mercy.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ukuzaji Biashara (DTP) Fortunatus Mhambe amesema kinachofanyika na TANZAKWANZA na TANTRADE ni jambo kubwa kwa lengo la kuinua biashara za wanawake nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com