Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SBL YAZINDUA KAMPENI YA 'JIBAMBE KIBABE' KUINUA MFUMO WA BIASHARA


Jonas Sindabaha, Msambazajii wa vinjwaji vya Kampuni ya Serengeti, akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya 'Jibambe Kibabe' ambayo imelenga kuwanufaisha wanaofanya nao biashara kwa ukaribu.
Nicholas Chonya, Meneja Mauzo wa Kanda wa Serengeti Breweries Limted akifafanua jambo juu ya kampeni 'Jibambe Kibabe' ambayo itahusisha vinywaji vyetu vyote vinavyotengenezwa na kampuni hiyo.
Irene Mutiganzi, Mkuu wa Masoko ya Vinywaji Vikali, Serengeti Breweries Limted akizugumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni yake kubwa ya kitaifa 'Jibambe Kibabe' inayolenga kuchochea uwezeshaji kiuchumi katika mfumo wake mzima wa biashara.

Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua kampeni yake ya kitaifa 'Jibambe Kibabe' inayolenga kuchochea uwezeshaji kiuchumi katika mfumo wake mzima wa biashara.

Kampeni hiyo itatoa motisha, marejesho ya fedha, na punguzo kwa washirika wake wa biashara wanaponunua bia na vileo vya SBL.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Julai 18, 2023 Mkuu wa idara ya Vileo kutoka SBL, Irene Mutiganzi, amesema, washindi wa kampeni ya 'Jibambe Kibabe' kutoka mtandao wa biashara wa SBL ni pamoja na wauzaji wakubwa, wauzaji jumla, wasambazaji na maduka ya rejareja.

"Kampeni ya 'Jibambe Kibabe' imeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha washirika wa kibiashara wa SBL, haswa katika mazingira ya uchumi ya sasa ambapo biashara zinakaribia kupona kutokana na kutokuwa na uhakika wa kiuchumi katika miaka kadhaa iliyopita." Amesema Mutiganzi.

Akifafanua kuhusu muundo wa kampeni hiyo, Mutiganzi amesisitiza kuwa kampeni hiyo inawapatia wateja wanaofanya vizuri punguzo na marejesho ya fedha, na pia kuwapa fursa ya kupata soko kutokana na athari inayotarajiwa ya kampeni hiyo inayosukuma ununuzi zaidi.

Aidha, kampeni hiyo pia inajumuisha kipengele kinachowazawadia wafanyakazi wa baa kwa kila chupa wanayouza kwa kufikia malengo yao.

Wengine wanaonufaika na 'Jibambe Kibabe' ni watumiaji katika kiwango cha baa ambapo kampeni hiyo imeandaa ofa za kubebea (bucket deals) zilizo tengenezwa maalum kwa watumiaji kufurahia na kushiriki na marafiki kwa bei iliyopunguzwa, hatimaye kutoa akiba kwa wote.

Naye, Nicholas Chonya, Meneja Mauzo wa Serengeti Kanda ya Dar es Salaam amesema kampeni hiyo itahusisha vinywaji vyetu vyote, kwa maana ya bia na baadhi ya pombe kali zinazotengenezwa na kampuni ya bia ya Serengeti.

"Nitoe wito na msisitizo kwa washirika wetu wa kibiashara, kuanzia wasambazaji mpaka mlaji wa mwisho, kushiriki kwa wingi," alisema Chonya na kuongeza.

"Kwa mfano kupitia kampeni hii, wauzaji wa baa wanaofikia asilimia 50 ya malengo yao ya mauzo watajipatia kiasi cha fedha kuanzia shilingi 100 kwa chupa moja ya bia, hadi Sh. 1,000 kwa chupa moja ya pombe kali."

Kwa upande wake mwakilishi wa wasambazi wa vinywaji vya Serengeti, Jonas Sindabaha, alisema anawapongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuandaa kampeni hii ya 'Jibambe Kibabe' ambayo imelenga kuwanufaisha wanaofanya nao biashara kwa ukaribu.

"Hii inatudhihirishia kuwa Serengeti ni washirika wetu wa kibiashara wa kweli, wanaojali maslahi yetu. Hivyo niwapongeze kwa hatua hii," alisema Sindabaha.

Mwisho

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com