SERIKALI imeshauriwa kuweka akili kubwa katika sekta ya kilimo kwa lengo la kuondokana na wataalamu wa kilimo na badala yake kuwepo kwa wakulima wataalamu ambao watasaidia kwa kiasi kukubwa katika kuinua uchumi wa nchi.
Katika wakati huu ni bora kukawa na mapinduzi ya kilimo kwani suala la kuwa na njaa katika nchi yeti ni la kujitakia wenyewe kwa kuwa tuna maeneo mengi na mabonde mazuri ambayo yanafaa kwa kilimo hapa nchini.
Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Foundation ya Mjini Kahama Khamis Mgeja wakati akiongea na Waandishi wa habari na kuongeza kuwa sekta ya kilimo kwa wakati huu ndio ambayo inaweza kumuinua mkulima kwa haraka.
Mgeja ambaye pia ni mmoja wa wakulima kwa sasa alisema kuwa baadhi ya wataalamu wamekuwa hawafanyi kazi kwa kujituma hali ambayo inafanya wakulima kutokupata mazao mengi kwani kama wakulima watafundishwa kilimo cha kisasa wataweza kujisimamia wenyewe na hivyo kuleta mapinduzi makubwa katika sekta hiyo.
Hata hivyo Mgeja alishauri pia baadhi ya shule za sekondari za kata ziwe na miochepuo ya kilimo ili kuondokana na wanafunzi wanapomaliza shule shule kuweza kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea ajira kutoka serikali ambazo zinachukua kundi dogo.
Alisema kuwa katika shule hizo wanaweza kujifunza vitu kama vile ufugaji, uvuvi pamoja na mambo mengine kwani ajiara zipo kwa wingi katika maeneo hayo na hivyo kuweza kujitegemea kuliko kusubiri ajira kutoka serikalini.
Alisema kuwa kilimo kinaweza kututoa katika umasikini kwa kutumia rasilimali tulizo nazo kama vile mabonde yenye rutuba. Mito na maziwa makubwa ambayo yanaweza kutumika katika kuzalisha mazao mbalimbali ambao wakulima waeza kulilisha hata Afrika kwa ujumla.
Akizungumzia kuhusu zao la Pamba Mgeja alisema kuwa zao limekuwa likishuka bei kila mwaka kutokana na hali iliyiopo katika soko a Dunia hali ambayo Mkulima anatumia nguvu kubwa huku akipata kipata kipato kidogo.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo ni bora serikali aikaweka kiwanda cha kimkakati hapa nchini na kuacha kuuza marobota nje ya nchi hali ambayo Mkulima anaweza kufaidika kupitia hali hiyo hiyo.
Alisema kuwa kama kiwanda kitakuwepo Pamba itaongezeka thamani kwa kiasi kikubwa huku akiishauri serikali kupitia Wizara husika kuona ni jnsi gani wanaweza kufanikisha suala hilo kwani kwa sasa mazao ya wakulima hayana thamani hususani zao hilo.
“Ninaishauri Serikali kujeng kiwanda kwa ajili ya kusindika pamba hata kwa kushirikiana na vyama vya ushirika huku kukiwa na lengo moja ya kuipandisha Pamba thamani na Mkulima kuweza kuifaidika kwa kile ambach atakuwa amelima”, Alisema Khamis Mgeja.