Watu sita wameuawa na mmoja kujeruhiwa katika tukio la kuchomwa kisu katika shule ya chekechea katika jimbo la Guangdong kusini-mashariki mwa China, polisi wameiambia BBC.
Polisi walisema wamemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 25 na wanachunguza chanzo cha shambulio hilo.
Hawajafichua maelezo yoyote kuhusu waathiriwa lakini wameiita kesi ya "shambulio la kukusudia".
Walisema shambulio hilo lilitokea Jumatatu saa 07:40 kwa saa za ndani (23:40 Jumapili GMT).
Mmiliki wa duka ambaye anafanya kazi karibu na shule ya chekechea aliambia BBC kuwa eneo jirani limefungiwa.
Lianjiang ina wakazi wapatao milioni 1.87.
Kadiri video za shambulio hilo zilivyoenea katika mitandao ya kijamii ya Uchina, zilizua hasira na mshtuko
CHANZO - BBC
Social Plugin