Wadau wa Madini wameridhishwa na uwepo wa madini mbalimbali katika banda la Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Katika banda hilo wadau wanaotembelea banda wanaelezwa kuhusu utambuzi wa madini ya Vito, uthaminishaji, elimu kuhusu ukataji, ung'arishaji madini ya vito na uzalishaji pamoja na uuzaji.
Aidha, Mjiolojia Cleophas Siame amewaeleza wadau kuwa kituo hicho kinatengeneza na kurekebisha bidhaa zitokanazo na madini hayo.
Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kinawakaribisha wadau wote kutembelea banda hilo ili kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo kusafishiwa pete, hereni na vidani vilivyochafuka, kutengenezewa hereni, pete za dhahabu, madini ya fedha (silver) na madini mengine ya Metali na Vito.