Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini Adv. Steven Byabato akiwapa pole waathirika wa mafuriko
Na Mwandishi wetu _ Malunde blog
Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini Adv. Steven Byabato leo Julai 3,2023 amewatembelea waathirika wa mafuriko katika Jimbo la Bukoba ambayo yalitokea mwishoni mwa mwezi Juni 2023 baada ya mvua kubwa kunyesha.
Baada ya kufika kwa waathirika hao wa mafuriko, mbunge Byabato amewapa pole wananchi waliokubwa na mafuriko na kusema kuwa kwa kuwa hakuwa jimboni wakati matatizo hayo yakitokea ilimlazimu kuomba ruhusa kwa viongozi wake ili aweze kufika jimboni kwake na kuwaona waathirika wa mafuriko.
Amesema kuwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali kwa ajili ya kutembelea maeneo ya waathirika wa mafuriko.
Wakati akizungumza na waathirika hao wa mafuriko baada ya kufika kata ya Bakoba amesema kuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kilio cha wana Bukoba kuhusiana na mto kanoni anakifahamu na ameazimia katika kipindi chake akimalize kilio hicho kwa kujenga kingo za mto Kanoni .
Aidha kingo hizo zitajengwa kwa upana, urefu ,mwinuko na kona ambazo hazitawaathiri wananchi ambapo tayari Mh Rais amesharuhusu tangazo la kumtafuta mkandarasi mshauri atakayeshauri namna ya kutengeneza kingo hizo za mto kanoni kwani maeneo ya mto huo yanatofautiana.
Social Plugin