Padri wa kanisa katoliki anayesimamia kanisa la ST Peters Ruai nchini Kenya amefariki dunia baada ya kurusha roho usiku akiwa na mpenzi wake katika hoteli moja mjini Murang'a.
Padri huyo ambaye ametambuliwa kwa jina Joseph Kariuki Wanjiku, mwenye umri wa miaka 43, alithibitishwa kufariki asubuhi ya Jumamosi, Julai 8, 2023 baada ya mpenzi wake kumkimbiza hospitalini.
Ripoti ya polisi inaonyesha kuwa wapenzi hao waliingia kwenye Hoteli ya Monalisa Delview huko Gatanga jioni ya Ijumaa, lakini alianza kujisikia vibaya kesho yake asubuhi.
"Kisha, asubuhi ya (Jumamosi) mwendo wa saa 0800, mpenzi wa padri huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa hoteli kuwa mpenzi huyo alikuwa ana kizunguzungu na kupoteza fahamu ili waweze kumkimbiza hospitalini. Kisha wakamkimbiza hospitali ya Kenol ambako alifikwa na mauti kuwasili," ripoti ya polisi ilisema kwa sehemu.
Kariuki alifikwa na mauti akiwa bado ndani ya gari lake ambalo lilikuwa limetumika kumpeleka hospitali.
Maafisa wa polisi walioitwa walipata mwili huo kwenye kiti cha nyuma cha gari ukiwa umefunikwa na shuka la hoteli na povu jeupe likitoka mdomoni na puani.
"Mwili ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya mater Nairobi chini ya uangalizi wa afisa wa polisi ukisubiri uchunguzi wa maiti na hatua zaidi za polisi," ripoti ya polisi ilisema.
Vyakula na vinywaji ambavyo wapenzi hao walichukua usiku wa kuamkia leo vimechukuliwa kwa uchambuzi zaidi huku uchunguzi ukiendelea, Taifa Leo liliripoti.
Ripoti ya polisi ilionyesha kuwa wawili hao walikuwa wamelala pamoja katika kituo hicho ambapo walikuwa wamelala usiku mmoja kabla ya kifo chake kwa njia isiyoeleweka.
Kulingana na ripoti ya Daily Nation, mfanyakazi wa hoteli alifichua kuwa marehemu alikuwa mteja katika hoteli hiyo kwa miaka miwili na kila mara alidai faragha.
CHANZO - TUKO NEWS