Wananchi na watendaji mbalimbali wa serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali,viongozi wa dini na Chama wakifanya usafi wa mazingira katika hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete yaliyofanyika kiwilaya
Na Sumai Salum - Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe.
Joseph Mkude amewaasa watu wa rika mbalimbali hasa kundi la vijana ambao ni nguvu kazi na taifa la kesho kuifahamu kwa kina historia ya taifa lao.
Mkude ameyasema hayo leo Julai 25,2023 katika maadhimisho ya siku ya mashujaaa iliyofanyika kiwilaya katika viwanja vya hospitali ya wilaya hiyo ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete yakihudhuriwa na watumishi wa ofisi zote za serikali,mashirika,vyama vya siasa,viongozi wa dini.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliyoenda sanjari na zoezi la kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapo, Mkude
amesema vijana wanapaswa kuendelea kusoma kila siku waijue historia ya taifa hili namna lilivyopiganiwa na baadhi ya watu kwa lengo la kuwatoa watu wake kuwa mateka na watumwa kisha wawe huru kuishi maisha yao na endapo wakijua historia hawatabadilishwa na watu wachache wenye malengo mabaya na kuwapotosha vijana ili kuacha msingi wa taifa wa kuilinda na kutunza amani.
Mkuu huyo wa wilaya amesema nchi ya Tanzania imekuwa na mashujaa ambao tangu vita ya pili ya dunia wamekuwa wakipigania taifa kwa lengo la kulinda mipaka yao tangu enzi za waasisi hayati Mwl.Julias Kambarage Nyerere na Abeid Aman Karume kabla ya uhuru,baada ya uhuru 1961 na hata baada ya Muungano hivyo watanzania wanaowajibu mkubwa kuhakikisha wanaienzi siku hii muhimu kwa taifa.
"Ndugu zangu itambulike kuwa tumeamua kushiriki siku hii walau kwa kufanya kazi ya usafi hapa hospitalini kwetu ili na sisi tutoe jasho kama mashujaa wetu hapo mwanzo walivyotoa jasho na hata wengi wao kumwaga damu na kupoteza maisha ili watanzania wengi nikiwemo mimi na wewe tuwe na amani na ndani ya mioyo yetu tuko tayari kuifia nchi yetu iwe na utulivu na kulinda amani ya mipaka yetu" ,ameongeza Mkude.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na mgeni rasmi wa siku ya mashujaa Mhe. Joseph Mkude akizungumza kwenye maadhimisho hayo katika viwanja vya hospitali ya Wilaya ya Kishapu ya Dr.Jakaya Mrisho Kikwete
Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe.Joel Ndettoson akizungumza kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa yaliyofanyika kiwilaya kwa kufanya usafi
Katibu wa Umoja wa wanawake Chama Cha Mapinduzi Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Grace Magere akizungumza
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Bw. Emmanuel Johnson Matinyi akisaini daftari la wageni la hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete siku ya kumbukumbu ya mashujaa
Viongozi wa dini na Chama Cha mapinduzi wakimsikiliza mgeni rasmi Joseph Mkude katika maadhimisho ya siku ya mashujaaa kiwilaya yaliyoambatana na zoezi la kufanya usafi wa mazingira wa hospitali ya Dk.Jakaya Mrisho Kikwete wilayani Kishapu
Watumishi wa idara mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe. Joseph Mkude siku ya kuenzi mashujaa wa Tanzania.
Wananchi na watendaji mbalimbali wa serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali,viongozi wa dini na Chama wakifanya usafi wa mazingira katika hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete yaliyofanyika kiwilaya
Social Plugin