Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga ameendelea kuwafikia Wajasiriamali Mkoani Shinyanga ambapo leo ilikuwa zamu ya Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga kupatiwa msaada wa Majiko ya Gesi 165 yenye thamani ya Shilingi Milioni 8.2 kwa ajili ya kuwarahisishia kazi katika shughuli zao na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa utunzaji mazingira kwa kutumia nishati mbadala.
Akizungumza wakati wa kukabidhi majiko 165 yakiwa yamejazwa gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 7,2023 katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Mayenga amesema lengo lake ni kuwafikia akina mama wajasiriamali 800 katika wilaya zote za mkoa wa Shinyanga.
“Tayari nimetoa majiko 250 kwa Mama Lishe Wilayani Kahama yenye thamani ya shilingi Milioni 12.5 , na Majiko ya Gesi kwa Mama Lishe 165 Shinyanga Mjini yenye thamani ya shilingi Milioni 8.25 na nitaendelea kutoa majiko ya gesi katika wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga lengo ni kuwafikia wanawake 800 kwa kuwapatia majiko ya gesi”,amesema Mhe. Mayenga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga
“Wajasiriamali hawa, mama lishe hawa nimewatafuta kwenye maeneo yao ya kazi bila kuangalia hawa ni wanachama wa CCM ama la kwani lengo langu ni kuona wanawake wanapata furaha. Hii ni sehemu ya kuonesha upendo kwa Wajasiriamali na Mama Lishe pamoja kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wanawake katika shughuli za kiuchumi na utunzaji mazingira kwa kutumia nishati mbadala sambamba kuwapunguzia gharama za kununua mkaa na nishati zingine”,ameongeza Mayenga.
“Nitaendelea kutoa majiko ya gesi 800 mkoa mzima. Majiko haya tayari yana gesi, nina dhamira ya kutoa kwa wananchi kile ninachokipata. Mambo mengine tunafanya kwa sababu ya utashi wetu binafsi lakini pia mambo anayohamasisha Mhe. Rais Dkt. Samia viongozi tufanye katika kuwaletea maendeleo wananchi. Mhe. Rais Samia anataka wabunge tufanye kazi ya kusaidia wananchi”,amesema Mhe. Mayenga
Sehemu ya majiko ya gesi yaliyotolewa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kwa wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge huyo ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuwa wazalendo kwa kuwapenda na kuwasemea mazuri. “Tuwapende viongozi wetu, tuwataje kwa wema, tuwaseme vizuri”.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Grace Bizulu amempongeza Mbunge Mhe. Lucy Mayenga kwa moyo wa upendo na wa pekee katika kusaidia wananchi.
“Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpatie. Kwa kweli Lucy Mayenga ana moyo wa pekee, ana moyo wa kutoa. Wabunge wote Shinyanga wangekuwa kama Lucy Mayenga tungefika mbali”,amesema Bizulu.
Katika hatua nyingine amewataka akina mama kuacha viburi kwa waume zao na kuhakikisha wanafuata maadili mema na kutunza familia ili kuepuka mmomonyoko wa maadili unaochochea vitendo vya ukatili wa kijinsia.
“Tumepoteza maadili hatufundishi watoto tuko Busy na majukumu watoto wanaharibika. Naomba tufanye majukumu ya kutafuta pesa na kutunza familia lakini pia Wanawake tusiwe na kiburi, lazima tufuate maadili, tuheshimu waume zetu kisa tuna vipato kuwazidi akina baba. Watoto wetu wanadanga, wamekuwa mashoga kwa sababu ya kukosa maadili”,amesema Bizulu.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Rehema Nhamanilo amesema Mbunge Lucy Mayenga anapaswa kupongezwa kutokana na mambo makubwa ambayo amekuwa akiyafanya kuwasaidia wananchi.
“Mhe. Lucy Mayenga amekuwa akifanya mambo makubwa, anafanya vitu vya ajabu ambavyo hatujavizoea kuviona”,amesema Nhamanilo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi amesema kitendo alichofanya Mbunge huyo kuwakumbuka mama lishe kinapaswa kuigwa kwani kimewapa raha akina mama.
“Haya ndiyo mambo ya wabunge wa CCM kuwapa raha watu waliowachagua badala ya kuwapa mawazo au manung’uniko. Mhe. Lucy Mayenga umefanya jambo zuri, huu ndiyo uimara na umahiri ulionao ndani ya CCM. Mambo mazuri unayofanya yanawafanya wananchi wakipende Chama Cha Mapinduzi. Tunataka CCM ilelewe na wenye kujituma na kujitoa”,amesema Majeshi.
Nao Mama Lishe hao waliopata majiko ya gesi wamemshukuru Mbunge huyo kwa kuwapatia majiko hayo ya gesi ambayo yatasaidia katika kazi zao lakini pia kutunza mazingira huku pia wakimshukuru kwa kuleta Madaktari Bingwa wa Macho ambapo wananchi wa Mkoa wa Shinyanga walipata huduma bure.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akipokelewa kwa shangwe na akina mama wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga alipowasili katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini kwa ajili ya kutoa msaada majiko ya gesi 165 kwa Mama Lishe hao. Picha na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akipokelewa kwa shangwe na akina mama wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga alipowasili katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini kwa ajili ya kutoa msaada majiko ya gesi 165 kwa Mama Lishe hao.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akipokelewa kwa shangwe kwa kubebwa na akina mama wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga alipowasili katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini kwa ajili ya kutoa msaada majiko ya gesi 165 kwa Mama Lishe hao.
Mama Lishe wakipiga picha (Selfie) na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga ambapo amewapatia majiko ya gesi 165
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga ambapo amewapatia majiko ya gesi 165 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga ambapo amewapatia majiko ya gesi 165
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga ambapo amewapatia majiko ya gesi 165
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga ambapo amewapatia majiko ya gesi 165
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga ambapo amewapatia majiko ya gesi 165
Sehemu ya majiko ya gesi yaliyotolewa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kwa wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akicheza na viongozi na Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga wakati akikabidhi majiko ya gesi kwa Mama Lishe
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa tatu kulia) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa nne kulia) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa nne kulia) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa pili kulia) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa pili kulia) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa pili kulia) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa tatu kulia) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mmoja wa Mama Lishe akitoa neno la shukrani baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kukabidhi majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mmoja wa Mama Lishe akitoa neno la shukrani baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kukabidhi majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Grace Bizulu akizungumza wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akigawa majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Asha Juma Kitandala akizungumza wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akigawa majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Sharifa Hassan Mdee akizungumza wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akigawa majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Rehema Nhamanilo akizungumza wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akigawa majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi akizungumza wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akigawa majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi akizungumza wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akigawa majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya Mama Lishe/Wajasiriamali wakiwa kwenye mkutano na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga
Sehemu ya Mama Lishe/Wajasiriamali wakiwa kwenye mkutano na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga
Sehemu ya viongozi wa UWT wakiwa kwenye mkutano na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga

Picha ya kumbukumbu Wajasiriamali na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga

Picha za kumbukumbu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Tazama Video
Social Plugin