Meya wa Manispaa ya Moshi, Zuberi Kidumo
Baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii inayodai kuwa Meya wa Manispaa ya Moshi, Zuberi Kidumo alipigwa na diwani wa Mji Mpya, Abuu Shayo baada ya kurushiana maneno katika kikao cha kamati ya mipango miji ya Halmashauri hiyo. Kidumo amekanusha kuwapo kwa tukio hilo.
Taarifa zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii juzi jioni zimedai katika kikao hicho kulijitokeza sintofahamu iliyosababisha meya huyo kupigwa.
Purukushani hiyo inadaiwa imesababisha askari wa halmashauri kuingilia kati na hata diwani Shayo alipotoka nje ya ukumbi alisikika akisema yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake, na hata akigombea kama mgombea binafsi atashinda.
Social Plugin