Mo Mlimwengu
Na Mwandishi wetu _ Muleba
Katibu Hamasa wa vijana na chipukizi Umoja wa vijana CCM wilaya ya Muleba mkoani Kagera Mo Mlimwengu amesema atahakikisha anashirikiana na vijana ili kuimarisha jumuia hiyo.
Mo Mlimwengu amesema hayo ikiwa ni siku chache zimepita tangu achaguliwe na wajumbe wa Jumuiya hiyo kuwa katibu hamasa wa vijana na chipukizi katika wilaya ya Muleba .
Amesema kuwa alipoambiwa kuhusu nafasi hii alijitafakari kwanza ili aone kama anaweza wanza aliaangalia majukumu ya kiongozi wa CCM ni yapi? akabaini kuna mambo kama matatu ambayo ni pamoja na kukijenga chama.
"Wakati Baraza linanipitisha kuna watu walikuwa tayari kufanya lolote wahakikishe Mo Mlimwengu anakuwa mshindi lakini kuna watu hawakuwa tayari kuona napata hiyo nafasi. Hao wachache ambao hawakuwa tayari ndio walionipa deni kubwa kuhakikisha nafanya kama ipasavyo",amesema.
Amewashukuru wajumbe wa Baraza is vijana wilaya ya Muleba kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu kwake na kusema wamesimama imara kwa ajili ya masrahi ya vijana wa Muleba .
Social Plugin