MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki kikao cha Baraza la Wazee wa Wilaya ya Ikungi na kuwapongeza kwa kuendelea kutoa ushauri na kusimamia maadili kwenye jamii na hivyo kutimiza usemi usemao utu uzima dawa.
Mtaturu ametoa pongezi hizo Julai 12 katika kikao hicho ambapo pia amewapongeza wazee hao kwa kuaminiwa kuongoza baraza hilo.
Mtaturu amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mambo mengi kwa ajili ya wazee.
Amewahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hasan imedhamiria kuboresha huduma mbalimbali ili kuboresha maisha ya wananchi.
Amewahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hasan imedhamiria kuboresha huduma mbalimbali ili kuboresha maisha ya wananchi.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Mzee Joseph Mkuki amemshukuru Mbunge Mtaturu kwa kushiriki nao kwenye kikao cha wazee na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ya kimaendeleo.
Pamoja na pongezi hizo wamempatia mbunge kero zao azifikishe bungeni ikiwemo Sera ya Matibabu ya Wazee.
Social Plugin