•
Benki ya Letshego Faidika ni taasisi mpya (#OneBank) kufuatia
kuunganishwa kwa taasisi ya kifedha ya Faidika na Benki ya Letshego
Tanzania
• Wateja wa Letshego waliweza kupata huduma mbalimbali za mikopo, akiba, malipo, bima na nyinginezo.
• Bw. Baraka Munisi ameteuliwa rasmi kuwa ‘Afisa Mkuu Mtendaji wa Tanzania’.
Taratibu
za kuunganisha taasisi mbili za kifedha za Letshego Tanzania, (Letshego
Tanzania Limited t/a “Faidika” na benki ya Letshego Tanzania)
umekamilika na kuzaliwa taasisi mpya ya kifedha ya Benki ya Letshego
Faidika "Letshego Faidika Bank".
Bodi
ya Wakurugenzi ya Letshego Group imemteua Bw Baraka Munisi kushika
wadhifa wa Afisa Mtendaji Mkuu Benki mpya ya Letshego Faidika. Bw.
Baraka Munisi alijiunga na ‘Faidika’ ambayo ilikuwa chini ya kampuni ya
Letshego mwaka 2018, na Mei, 2019, aliteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu
wa ‘Faidika’ mwaka mmoja baadaye.
Ndani
ya miaka mine chini ya uongozi wa Bw Baraka, taasisi ya Faidika iliweza
kuongeza maradufu shughuli za mikopo midogo midogo, kuongeza ufanisi wa
uendeshaji na kuwa taasisi ya kwanza ya Microfinance Tanzania kupata
leseni ya daraja la pili (II) ya kuchukua amana.
Bw
Simon Jengo ambaye ni mwenyekiti mpya wa bodi ya Benki mpya ya Letshego
Faidika, amethibitisha uteuzi wa Bw Munisi kuwa Afisa Mtendaji Mkuu.
Jengo alisema "Utendaji wa Letshego nchini Tanzania utafungua fursa
nyingi za wadau na sasa tunaweza kuongeza ufanisi wa biashara, huku
tukiwapa wateja wetu machaguo mbalimbali ya bidhaa zetu ambazo ni
matokeo ya kuunganisha taasisi hizi mbili.
Kupitia uongozi wa Bw. Baraka katika taasisi ya Faidika na hasa kwa kuzingatia taaluma na uzoefu wake wa kitaifa na kimataifa, tunatarajia malengo yetu yanatafanikiwa na kufanya mageuzi makubwa na maendeleo ya biashara nchini Tanzania.”
Kupitia mazingira mazuri ya uwekezaji nchini na utendaji kazi wa taasisi hii mpya, tunarajia kudumisha na kuendeleza kauli mbiu ya Benki ya Letshego Faidika ya #ImaraPamoja au #StrongerTogether.
"Ni heshima kubwa kupata fursa ya kuendelea kuongoza taasisi ya Letshego Tanzania kupitia awamu nyingine yenye lengo la kukuza na utoaji huduma bora kwa wateja wetu nchi nzima. Tutaendelea kutumia rasilimali za biashara zote mbili ili kufikia malengo yetu ya kuboresha maisha ya Watanzania.
Hakika
sisi tupo #ImaraPamoja, imara kama timu iliyoungana na shukrani kubwa
zaidi kwa ushirikiano wa kimkakati tulioanzisha na mashirika mbalimbali
ya Tanzania.
Mkakati
wa Benki ya Letshego Faidika unabaki kuwa ule ule wa kuleta ukuaji
endelevu wenye ufanisi mkubwa wa kijamii kwa vizazi vijavyo," alisema Bw
Munisi ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu mteule wa Tanzania wa Benki ya
Letshego Faidika.
Uwepo
wa benki ya Letshego Faidika utaendeleza shughuli zao mbalimbali za
Letshego ambazo ni ukopeshaji, akiba, bima, malipo na mtindo wa maisha
ambapo ambapo wateja watakuwa na fursa ya kupata huduma mbalimbali kwa
njia za kisasa zaidi kupitia tovuti, USSD, huduma za simu za mkononi na
WhatsApp).
“Taasisi
yetu ya Afrika Mashariki itafaidika kutokana na kuunganishwa kwa taasisi
hizi mbili na kuwa taasisi moja yenye dira na madhumuni ya kuleta
ufanisi wa kifedha na fursa kwa Watanzania popote.
Kama
shirika la Afrika nzima, uboreshaji wa duduma mbalimbali endelevu
unabakia kuwa muhimu katika kuimarisha biashara na kuendelea kutoa
thamani kwa wateja wetu katika nchi 11 barani Afrika,” alisema Fergus
Ferguson, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kanda ya Masoko ya Mashariki na
Magharibi wa Letshego Group.
Ujumuishaji
wa mashirika mawili ya Letshego katika Benki ya Letshego Faidika
unaanza kutoka 04 Julai 2023, huku timu za eneo na nchi za chapa hiyo
zikiwa zimeunganisha mifumo, mitandao, utawala na bidhaa zote kwa muda
wa miezi 18 iliyopita. Wateja sasa wanaweza kufikia chaguo pana zaidi
katika bidhaa, na wanaweza kutazamia matoleo ya kusisimua zaidi katika
siku zijazo.
Kwa sasa
Watanzania watashuhudia ubadilishaji wenye maboresho makubwa ya matawi
na maduka ya Letshego na kuwa na muonekano mpya wa rangi ya njano na
nyeusi ambayo ni rangi halisi ya benki ya Letshego Faidika ikiwa na
kauli mbiu ya #ImaraPamoja ikiwa na nembo ya yenye rangi ya njano na
pembetatu a ‘tripod’ inayoashiria uaminifu, usaidizi na ukuaji. Matawi
na sehemu za kutolea huduma pia yataunganishwa au kuhamishwa ili
kuongeza urahisi kwa wateja upata huduma bora mbalimbali za mfumo wa
kidigitali.
WASIFU WA BW BARAKA MUNISI
Bw.
Baraka Munisi alijiunga na Letshego kwa mara ya kwanza mwaka wa 2018
akiwa kama Mshauri kiongozi, na mwaka 2019, aliteuliwa kuwa Afisa
Mtendaji Mkuu wa taasisi ya kifedha ya Faidika chini ya kampuni ya
Letshego. Chini ya uongozi wa Bw Munisi, Taasisi ya Faidika iliongeza
faidi maradufu huku ikipnguza gharama mbalimbali kwa njia ya utendaji
kazi ulioimarishwa na kuwa taasisi ya kwanza ya Taasisi ndogo ya Fedha
Tanzania kupata leseni ya kuweka amana ya daraja la II.
Bw
Munisi pia alifanikiwa kuleta uzoefu wa kimataifa wa masuala ya fedha
na kibenki kwa zaidi ya miaka 18 katika jukumu lake jipya ambapo
aliupata akiwa mfanyakazi katika mashirika kadhaa ya umma na kimataifa.
Kabla ya kujiunga na Letshego, Bw Munisi aliwahi kufanya kazi katika
kampuni mbalimbali ambazo ni Freddie Mac USA ambayo ni moja ya ya
mashirika mawili ya Serikali ya Marekani, JP Morgan Chase USA, Wells
Fargo USA, Benki ya Dunia; na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Katika
kipindi chake katika Benki ya Dunia Bw. Munisi alichukua jukumu muhimu
katika kuanzisha kituo cha kwanza cha ukwasi wa mikopo ya nyumba katika
Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, kiitwacho Tanzania Mortgage
Refinance Company (TMRC).
Akiwa
Benki Kuu ya Tanzania Bw. Munisi alihusika na utekelezaji wa Mradi wa
Kitaifa wa Fedha kwa ajili ya makazi. Pia alikuwa muhimu katika
kuanzisha mpango wa kitaifa wa makazi ya watumishi wa umma, chini ya
agizo la Rais wa Tanzania wakati huo, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete. Baada ya hapo alisaidia uanzishwaji wa ‘Watumishi Housing’,
taasisi inayomilikiwa na Serikali inayomilikiwa na Mfuko wa Pensheni wa
Tanzania ili kutoa nyumba za gharama nafuu kwa watumishi wa umma.
SIFA: (ELIMU)
Bw
Munisi kwa sasa ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Biashara,
fedha na Makazi aliyohitimu katika Chuo cha Biashara cha Kogod Schools
of Business and International Management in Washington DC); Pamoja na
shahada zingine toka Chuo cha Wharton Business School of Real Estate
Pennsylvania Philadelphia; Boulder institute of Microfinance Turin,
Italia; Chuo Kikuu cha Frankfurt, Ujerumani.