Paroko wa Kanisa la Katoliki, Parokia ya Karatu mkoani Arusha, Pamphili Nada ameuwa kwa kupigwa na kitu kizito na mtu anayedaiwa kuwa na matatizo ya afya ya akili aliyeingia Kanisani kwa nguvu kutaka kusali.
Hata hivyo baada ya mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Romani Leonard (30) kufanya mauaji hayo naye ameuawa na Wananchi wenye hasira.
Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo leo Jumatano Julai 19, 2023.
"Padri alifariki wakati anapelekwa hospitali na mtuhumiwa aliuawa na wananchi wenye hasira baada ya kupata taarifa za tukio hilo,"amesema.
Social Plugin