Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI SHINYANGA WAKAMATA MTANDAO WAUAJI 'WAKATA MAPANGA' , BUNDUKI ZA MAKAMPUNI ZIKIAZIMWA


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu akionesha vifaa vya kupigia ramli chonganishi vilivyokamatwa

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kubaini na kukamata mtandao wa wakata mapanga wanaowakodisha ili kutekeleza mauaji huku likikamata bunduki nne zilizokuwa zikitumika katika Makampuni ya ulinzi na kuazimana kinyume na sheria.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Julai 26,2023, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu amesema bunduki hizo zimekamatwa kufuatia misako na Operesheni mbalimbali zilizofanyika katika kipindi cha Mwezi mmoja kuanzia tarehe 22/06/2023 hadi tarehe 25/07/2023 kwa lengo la kuzuia uhalifu ili kuendelea kuuweka Mkoa katika hali ya utulivu.


“Kupitia taarifa fiche tumefanikiwa kubaini na kukamata mtandao wa wakata mapanga wanaowakodisha ili kutekeleza mauaji. Tumekamata watuhumiwa wanne. Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa wamehojiwa na wamekiri kutenda matukio hayo sehemu mbalimbali, Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea na msako mkali kwa kushikiana na Mikoa jirani ili kuhakikisha linaukamata mtandao wote wa wakata mapanga”,ameeleza Nyandahu.


“Pia tumefanikiwa kukamata Bunduki 04 ambazo ni MARK IV yenye namba D.6000, MARK III yenye namba C.3667, MARK III yenye namba K.9234, Shotgun yenye namba 10737 ambazo zilikuwa zikitumika katika Makampuni ya ulinzi na kuazimana kinyume na Sheria, zimekamatwa risasi 73 za Shotgun, maganda 13 ya sisasi za shotgun, Risasi za Pisto 239, Pikiki 02, Bangi Kilo 2 na kete 02, Cappet vipande 02, na Waya wa Fensi Mita 12 mali idhaniwayo kuwa ya Mgodi wa Buzwagi, Mafuta ya Disel Lita 310 yaliyoibiwa katika mradi wa Reli SGR, na Vifaa vya kupiga Ramli chonganishi”,amesema Nyandahu.


Amesema katika kipindi hicho cha Mwezi mmoja kesi 33 za makosa ya Jinai zikiwa na jumla ya washitakiwa 41 ziliweza kupata mafanikio mbalimbali Mahakamani ambapo kesi moja kati ya hizo ya kujeruhi mtuhumiwa alihukumiwa miaka 10 Jela na akitoka alipe pesa Tshs. 100,000/=.

Amefafanua kuwa katika kuendelea kudhibiti matukio hatarishi ambayo yanayosababisha ajali za mara kwa mara kikosi cha Usalama barabani Mkoa wa Shinyanga kimeendelea kutoa elimu ya Usalama barabarani kwa makundi mbalimbali kupitia vijiwe vya pikipiki (bodaboda), nyumba za ibada (kanisani na misikitini), na kupitia Radio zilizopo Mkoani Shinyanga, shule za misingi na Sekondari, kwenye mikusanyiko mfano minadani.


“Hata hivyo Operesheni ya kukamata madereva wanaokiuka Sheria za Usalama Barabarani kwa makosa ya mwendokasi kwa kutumia Speed Radar na mfumo wa ufuatiliji wa Mwendo kwa mabasi ya abiria VTS (Vehicle Tracking System) inaendelea na mpaka sasa jumla ya pikipiki 882 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ubovu wa pikipiki, kutovaa kofia (Helmet), kutokuwa na Leseni, kutokuwa na bima, na kuzidisha abiria.

 Magari 3,423 yalikamatwa kwa makosa mbalimbali kati ya hayo magari 673 yalikamatwa kwa kuendeshwa kwa mwendokasi na hatarishi kwa kutumia Speed Radar na VTS, Madeva 673 waliandikiwa faini za barabarani kwa magari yaliyoendeshwa kati ya 80kph na 89kph”,amesema Nyandahu.


Amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linatoa wito kwa wananchi wake kufuata Sheria za nchi na kutojihusisha na vitendo vya kiuhalifu, kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, na litaendela kuwachukulia hatua kali za Kisheria kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo uhalifu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Julai 26,2023
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu akionesha bunduki zilizokamatwa
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu akionesha bunduki zilizokamatwa
Vifaa vilivyokamatwa na jeshi la Polisi
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu akionesha mali mbalimbali zilizokamatwa
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu akionesha mali mbalimbali zilizokamatwa
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Leonard Nyandahu akionesha mali mbalimbali zilizokamatwa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com