UWT SHINYANGA VIJIJINI YATOA TAARIFA YA KAZI MIEZI SITA, DKT. MZAVA ACHANGIA TOFALI 200 UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU


Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Vijijini ,Magdalena Dodoma akisoma taarifa ya kazi miezi sita (Januari hadi Juni) kwenye kikao cha baraza la Wajumbe lililofanyika kwenye ukumbi mdogo Jengo la CCM Mkoa leo Juni 08 2023.

Na Halima Khoya - Shinyanga.

Umoja wa Wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Shinyanga vijijini yatoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na Taarifa ya kazi kwa miezi sita (Januari hadi Juni 2023) ili kujadili miradi ya maendeleo, changamoto na kuwasilisha taarifa za Kata ili kujua uhai wa Jumuiya.

Akisoma taarifa ya Wilaya Shinyanga vijijini Katibu wa UWT ,Magdalena Dodoma amesema Wilaya hiyo ni miongoni mwa Wilaya zinazounda Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na Kahama,Kishapu, na Shinyanga mjini.

“Wilaya ya Shinyanga vijijini ina jimbo moja la uchaguzi,Tarafa tatu,Kata 26,Matawi 141,Vijiji 126 na Vitongoji 558",amesema Dodoma.

Hata hivyo, Dodoma amesema kuwa UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini ina jumla ya viwanja viwili ambavyo ni kiwanja cha kujenga nyumba ya katibu ambayo maandalizi ya kuanza ujenzi yanaendelea na kiwanja cha kujenga mashine ya kusaga na kukoboa.

Akizungumza kwa njia ya simu na Wajumbe wa Baraza,Mbunge wa Jimbo la Shinyanga vijijini,Ahmed Salum amewapongeza Wanawake wa UWT kwa ushirikiano wao wa kujenga jumuiya ambapo ameahidi jumuiya kuisaidia pale itakapo hitaji msaada wake.

pia Mheshimiwa amewezesha ukarabati wa ofisi ya UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava ameipongeza UWT kwa jitihada za kukuza jumuiya hiyo huku akiahidi kuchangia matofali 200 kwenye ujenzi wa nyumba ya Katibu ili kuendeleza jitihada zinazofanywa na UWT katika Wilaya hiyo.

Aidha kwa upande wake Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga amewaahidi wajumbe kufikia  Septemba 2023 wataenda Dodoma ikiwa ni mkakati wa kutimiza ahadi yake.
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Vijijini ,Magdalena Dodoma Akisoma na kutafsiri kanuni ya uwt kuhusu  kazi za baraza la Uwt wilaya kifungu Na 59(1) kwenye kikao cha baraza la Wajumbe lililofanyika kwenye ukumbi mdogo Jengo la CCM Mkoa leo Juni 08 2023.
Christina Mzava Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga akizungumza na wajumbe wakati wa kikao cha baraza kikiendelea kilichofanyika  kwenye ukumbi mdogo Jengo la CCM Mkoa leo Juni 08 2023.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Lucy Mayenga akizungumza na wajumbe wakati wa kikao cha baraza kikiendelea kilichofanyika  kwenye ukumbi mdogo Jengo la CCM Mkoa leo Juni 08 2023.
Umoja wa Wanawake Wilaya ya Shinyanga Vijijini (UWT) wakiendelea na baraza lililofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa Shinyanga leo Juni 08 2023.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post