Mchezaji wa Geita Gold FC George Wawa ametembelea kituo cha kulelea watoto waishio mazingira magumu cha MOSA wilayani Manyoni.
Wawa ambaye ni mwenyeji wa Wilayani Manyoni ametumia muda huo wa likizo kwa kuungana na Wazazi wake pamoja na viongozi mbalimbali wa michezo akiwemo Mkurugenzi wa Taasisi ya MYESAO Inj. Aidan Mlalo pamoja na Mkurugenzi wa ufundi wa Mlimani Academy Bw. Luca Mdachi ambapo Mchezaji huyo alipitia Academy hiyo katika timu ya vijana.
Wawa amesema ameona ni vyema katika likizo yake kuwatembelea wahitaji hao na kuwapelekea mahitaji mbalimbali na kuonesha upendo.
Naye, Mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Mahewa Mowo amemshukuru na kumpongeza mchezaji huyo kwa kuchagua fungu hilo la kurudisha fadhila kwenye jamii aliyotoka hususan kwa watu wenye uhitaji
Social Plugin