Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZEE, MACHIFU NA VIONGOZI WA KAMATI YA AMANI NA MARIDHIANO SHINYANGA WALAANI VIKALI WAOTUKANA VIONGOZI WA TAIFA SAKATA LA BANDARI, WATOA NENO WABUNGE KUKAA KIMYA

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga, Sheikh Balilusa Khamisi.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wazee, Machifu na Viongozi wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga wametoa tamko la kupinga na kulaani vikali kitendo cha baadhi ya wananchi na wanasiasa kutumia lugha zisizokuwa na staha dhidi ya viongozi wa taifa kuhusu uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam badala yake wajadili kwa kujenga hoja, kushirikiana na viongozi kwa kutoa maoni yanayoweza kujenga na kutunza amani ya taifa.

Tamko hilo limetolewa leo Jumamosi Julai 8,2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga, Sheikh Balilusa Khamisi kwa niaba ya Wazee, Machifu na Viongozi wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga.

"Katika kikao chetu leo tarehe 08.07.2023 tumejadili mambo mbalimbali yanayoendelea katika nchi yetu ikiwemo mapokeo hasi kwa baadhi ya wananchi na wanasiasa kuhusu mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai, Falme za Kiarabu kuhusu Ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha utendaji kazi Bandari Tanzania",amesema Sheikh Balilusa.

"Baadhi ya wananchi na wanasiasa wamekua na tafsiri potofu dhidi ya mkataba huo kwani wamekua wakitumia lugha zisizo na staha, maneno ya uchochezi, maneno yanayoondoa umoja katika Taifa, maneno yanayodhihirisha chuki binafsi na kuonesha nia ovu kwa Mhe. Rais pamoja na kudiriki kumtukana Mhe. Rais kwa hoja zao binafsi na kutamka maneno machafu kwa viongozi wa Taifa letu",ameongeza.

Sheikh Balilusa ameeleza kuwa Serikali ilitoa ruhusa kwa wadau kuendelea kutoa maoni yao na kwamba maoni hayo yatazingatiwa. Lakini baadhi ya wanasiasa badala ya kutoa maoni yao, wamekuwa wakitoa kauli na Lugha zisizokuwa na staha kwa viongozi wa Taifa na kupelekea kudhihirisha nia zao ovu kwa Taifa kwani vitendo vyao vinapelekea taharuki kwa umma jambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

"Hivyo basi kupitia kikao chetu tunatoa tamko kwamba, sisi Wazee, Machifu na Viongozi wa kamati ya amani na maridhiano Mkoa wa Shinyanga hatukubaliani, tunapinga na tunalaani vikali kitendo cha baadhi ya Wananchi na Wanasiasa kutumia Lugha zisizokuwa na staha dhidi ya viongozi wa taifa badala yake wajadili kwa kujenga hoja, kushirikiana na viongozi kwa kutoa maoni yanayoweza kujenga na kutunza amani ya taifa letu na Serikali itapokea maoni yao kama ilivyoahidi",amesema Sheikh Balilusa.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga, ametumia fursa hiyo kuwataka Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya mikutano ya hadhara wazungumzie usahihi wa suala la Uwekezaji katika Bandari ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na baadhi ya wananchi na wanasiasa.

"Bunge limemaliza vikao vyake, Wabunge waache kukaa kimya wafanye mikutano ya hadhara ili kutoa ufafanuzi kwa wananchi kwa sababu wabunge wanalijua vizuri suala hili na wao ndiyo walipitisha azimio la kuridhia Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania. Wabunge na viongozi wa Chama wafanye mikutano ya hadhara waeleze usahihi wa jambo hili kuepuka upotoshaji",ameongeza Sheikh Balilusa.

Juni 16, 2023 Baraza la wazee, viongozi wa dini na Machifu Mkoani Shinyanga walitoa tamko la kuunga mkono makubaliano ya uwekezaji kwenye bandari ya Dar es salaam kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya DP World wenye lengo la kuanzisha ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini.

Tamko hilo lilikuja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha azimio la kuridhia Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga, Sheikh Balilusa Khamisi akisoma Tamko la Wazee, Machifu na Viongozi wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga kupinga wanaotoa maneno yasiyokuwa na staha kwa baadhi ya Viongozi wa Taifa juu ya suala la uwekezaji wa Bandari nchini.

Chifu Kidola II Charles Njange ambaye ni Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Shinyanga na Katibu wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati Wazee, Machifu na Viongozi wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga wakitoa tamko la kupinga wanaotoa maneno yasiyokuwa na staha kwa baadhi ya Viongozi wa Taifa juu ya suala la uwekezaji wa Bandari nchini.

Mzee Zengo Mikomangwa akizungumza wakati Wazee, Machifu na Viongozi wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga wakitoa tamko la kupinga wanaotoa maneno yasiyokuwa na staha kwa baadhi ya Viongozi wa Taifa juu ya suala la uwekezaji wa Bandari nchini.
Mzee Juma Alley akizungumza wakati Wazee, Machifu na Viongozi wa Kamati ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Shinyanga wakitoa tamko la kupinga wanaotoa maneno yasiyokuwa na staha kwa baadhi ya Viongozi wa Taifa juu ya suala la uwekezaji wa Bandari nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com