Na Mariam Kagenda -Muleba
Kikundi cha Whatsapp kinachoitwa Muleba Breaking News kimetoa msaada wa kiwanja na mahitaji mbalimbali ya nyumbani kwa mama Leonida Brasio ambaye alifiwa na watoto wake wawili ambao waliopoteza maisha baada ya kuangukiwa na kufukiwa na mawe wakati wakichimba mchanga .
Wakitoa msaada huo Mohamed Isumail, Suleiman Zuku na Ridhiwani Samadu ambao ni wanakikundi hicho wamesema lengo la kutoa msaada huo ni baada ya kuona maisha anayoishi mama huyo ambapo watahakikisha anaondokana na changamoto ya upweke ili aweze kuishi kama wanawake wengine.
Wameongeza kwa kuwasihi wadau wengine wa maendeleo kuendelea kumsaidia mama huyo kwani anapitia wakati mgumu wa kupoteza watoto wake wote wawili.
Naye mama huyo Leonida Brasio ameshukuru kwa msaada wa kiwanja alichopatiwa kwani maisha anayoishi kwa sasa ni magumu na hana mahala pa kuishi ambapo ameomba wadau mbalimbali kuendelea kumsaidia kwani watoto wake ndiyo walikuwa wakimsaidia kupata ridhiki ya kila siku kupitia shughuli zao za uchimbaji wa mchanga.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Magata, Kashimili Kahauza mekishukuru kikundi hicho cha Whatsapp kwa msaada wa kumnunulia kiwanja kwani hakuwa na makazi maalum ya kuishi ambapo ameahidi kuhakikisha anahamasisha wananchi wanamjengea nyumba mama huyo lengo ni kuhakikisha anaondokana na changamoto anazokabiliana nazo kwa sasa
Social Plugin