MAHAKAMA kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu Idris Mwakabola kunyongwa hadi kufa, baada ya kupatikana na hatia ya kumnyonga Happiness Mbonde, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mwakabola alifikia uamuzi wa kumuua mpenzi wake huyo kwa kuhisi ana uhusiano na mwanamume mwingine. Kabla ya kufanya kitendo hicho, alimwingilia kimwili mpenzi wake huyo bila ridhaa yake kisha kumpa kinywaji chenye kilevi na hatimaye kumnyonga.
Akisoma hukumu hiyo juzi, Jaji Ephery Kisanya, alisema maelezo yanaonyesha kuwa Mwakabola alimuua Happiness baada ya kupata hasira na kwamba kifungu cha 201 cha Kanuni ya Adhabu itatumika, lakini pia maelezo hayo lazima yathibitishe kuwa mauaji yalifanyika wakati mshtakiwa alipokuwa na hasira.
"Lakini lazima mshtakiwa ahojiwe wakati ule ule baada tu ya tukio. Kwa shauri hili, Happiness hakuuawa pale pale baada ya mshtakiwa kuona amepigiwa simu na mpenzi wake wa zamani. hakuna kinachoshawishi kwamba aliuawa kwa hasira, bali inaonyesha Idris (Mwakibola) alidhamiria,” alisema Jaji Kisanya.
Social Plugin