Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Dkt. Oscar Kikoyo
Na Mariam Kagenda _ Muleba
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Dkt. Oscar Kikoyo amesema ataendelea kuwasemea wananchi wa jimbo hilo katika kipindi chake cha uongozi ili kuhakikisha changamoto zilizopo kwenye maeneo yao zinatatuliwa hasa kwa kuhakikisha wanapata huduma bora za afya,Elimu na miundombinu ya barabara .
Dkt. Kikoyo amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Muleba katika mkutano wake wa adhara uliofanyika julai 7 mwaka huu katika eneo la kariakoo lililopo kata ya Muleba .
Amesema kuwa kazi ya mbunge ni kwenda kuwasemea wananchi wake na kutetea Jimbo ambapo katika kipindi cha uongozi wake kwa miaka 3 yapo mambo mengi ya maendeleo ambayo yamefanyika katika Jimbo hilo la Muleba kusini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya 8 ambazo tayari zimeshasajiliwa na watoto wameshaanza kusoma na serikali imeshaleta walimu .
Ameongeza kuwa pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapenda sana wananchi wa jimbo hilo na mwaka huu shilingi milioni 650 zimeshaletwa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na kununua vifaa tiba .
Aidha amesema kuwa yy kama mbunge wa Jimbo hilo wananchi waendelee kumpa muda wa kutimiza yale aliyoyahaidi na atahakikisha changamoto zilizopo zinafanyiwa kazi.