Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JESHI LA POLISI LAONYA WATU WANAOVAA MAVAZI YANAYOFANANA NA SARE ZA MAJESHI LA ULINZI NA USALAMA


Jeshi la Polisi Tanzania limewataka watu wote wenye tabia ya kuvaa mavazi yanayofanana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama kinyume na sheria za nchi, kuacha tabia hiyo mara moja kwani halitasita kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Jeshi hilo limesema katika siku za karibuni kumeibuka makundi ya watu, kampuni binafsi za ulinzi na baadhi ya walinzi wa viongozi wakivaa mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na Usalama

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa Sheria ya Kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu cha 178, kinakataza mtu yeyote ambaye si askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kuvaa sare za majeshi ambapo ameongeza kuwa sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 kifungu cha 6, inakataza pia.

Aidha Misime ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Tanzania linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelee kuiweka nchi salama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com