Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WIKI YA MWANANCHI YAMALIZIKA KWA SHANGWE YANGA IKIICHAPA KAIZER CHIEFS



KILELE cha ‘Wiki ya Mwananchi’ kimefikia tamati leo Julai 22,2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mashabiki wa Yanga kushuhudia burudani mbalimbali za wasanii ikiwemo kikosi chao chote cha msimu wa 2023/2024 na kumalizia Mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs kutoka nchini Afrika Kusini.

Katika tamasha hilo ambalo limefanyika kwa msimu wa tano tangu lilipoazishwa rasmi mwaka 2019, ni miongoni mwa matukio makubwa ambayo yamekuwa yakiteka hisia kwa mashabiki mbalimbali wa timu hiyo nchini.

Majira ya saa moja Mchezo kati ya wenyeji Yanga SC na Kaizer Chiefs ulianza kwa kasi huku Yanga wakionyesha burudani ya hatari huku wachezaji wake wapya Skudu Makudubela na Max Nzengeli wakiteka Shoo.

Mnamo dakika ya 45 +1 Yanga walipata bao kupitia kwa Mshambuliaji wao Kennedy Musonda akimalizia pasi safi kutoka kwa winga hatari Max Nzengeli

Kipindi cha Pili Yanga walirudi uwanjani wakiwa wamebadilisha kikosi chote usipokuwa mlinda mlango wao Metacha Mnata.

Yanga waliendelea kuonyesha kandanda safi na kuwaburudisha mashabiki waliofurika katika uwanja wa Benjamin Mkapa.



Hadi dakika 90 zinamaliza Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Kaizer Chiefs sasa Yanga wataendelea na mazoezi kujiwinda na Mchezo wa ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC kutafuta kuingia Fainali mchezo utakaopigwa Agosti 9,2023 uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com