Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Julai 26,2023- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Julai 26,2023
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na waandishi wa habari
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenge wa Uhuru utapokelewa Mkoani Shinyanga ukitokea mkoani Simiyu Alhamisi Julai 27,2023 ukitarajiwa kuweka Mawe ya Msingi, kufungua na kuona jumla ya Miradi 41 yenye thamani ya Shilingi 14,027,687,009.20.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Julai 26,2023 , Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema Mwenge wa Uhuru utapokelewa katika shule ya msingi Buganika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
“Katika Mkoa wa Shinyanga Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa kilomita 571.5 ambapo utaweka Mawe ya Msingi, kufungua na kuona Jumla ya Miradi 41 yenye thamani ya Shilingi 14,027,687,009.20”,amesema Mhe. Mndeme.
“Katika Miradi hiyo,Miradi 11 itawekewa Mawe ya Msingi ikiwa na thamani ya Shilingi 7,841,516,050.00, Miradi 14 Itazinduliwa ikiwa na thamani ya Shilingi 3,308,062,056.20, Miradi 4 Itafunguliwa ikiwa na thamani ya Shilingi 1,321,826,665.00 na Miradi 12 Itaonwa ambayo inathamani ya Shilingi 1,556,282,238.00”,ameongeza.
Amefafanua kuwa Miradi hiyo imegharamiwa na Serikali Kuu Shilingi 8,740,635,261.40 huku Halmashauri zikichangia Shilingi 3,921,724,028.00 bila kusahau nguvu za wananchi shilingi 116,464,744.80 ,Sekta binafsi na Wahisani mbalimbali 1,248,862,975.00.
“Nichukue fursa hii kuwaalika na kuwakaribisha Wananchi wote katika maeneo yote ambayo Mwenge wa Uhuru utapita ikiwemo sehemu ya kuupokea, Mkesha, na kwenye miradi yote wananchi mjitokeze kwa wingi katika maeneo hayo”,amesema Mndeme.
Ameyataja maeneo ya mkesha wa mwenge wa Uhuru kuwa ni Uwanja wa Stendi ya Mabasi Maganzo (Kishapu), Uwanja wa Sabasaba (Manispaa ya Shinyanga), Uwanja wa Shule ya Msingi Didia (Halmashauri ya Shinyanga), Kituo cha Uwekezaji Nyihogo (Manispaa ya Kahama), Uwanja wa Mseki – Bulungwa (Ushetu) na Uwanja wa Shule ya Msingi Kakola A (Msalala).
Social Plugin