NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AAGIZA MKANDARASI ALIYEKULA PESA KISHA KUKIMBIA MRADI KIJIJI CHA MWANINGI ACHUKULIWE HATUA

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maji nchini Mhandisi Cyprian Luhemeja amemtaka mkandarasi anayefahamika kwa jina la PET aliyekuwa akitekeleza ujenzi wa mradi wa tanki la kuhifadhia maji lililopo kijiji cha Mwaningi kata ya Buligi halimashauri ya Msalala Wilayani Kahama wenye thamani ya shiringi bilioni 2.2 kuripoti kwa mkuu wa wilaya hiyo mara baada ya kutelekeza ujenzi wa mradi huo.

Ametoa kauli hiyo Julai 22, 2023 wakati wa ziara yake ya ukaguzi ikiwa ni muendelezo wa ziara ya ukukagua ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maji, uendeshaji wa mamlaka za maji na ubora wa utoaji wa huduma kwa wateja mkoani Shinyanga.

Ambapo amemtaka mkandarasi huyo kurudisha kiasi cha fedha alichokuwa amechukua na kuripoti kwa mkuu wa wilaya ya Kahama ifikapo jumatatu, na kumuagiza meneja wa Mamlaka ya Mji safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA mkoani Shinyanga kuvuja mkataba wa ujenzi walioingia na mkandarasi huyo.

“Hatuwezi kuvumilia mambo ya namna hii, aliomba na akapatiwa malipo ya awali kiasi cha shilingi milioni 366 lakini bado amekimbia na kutelekeza mradi, na mradi huu ulitakiwa ukamilike mwezi 6, 2023 na mpaka sasa uko chini ya asilimia 29, na ukiangalia eneo hili linalozunguka mradi huu wananchi wanachangamoto ya huduma ya maji, hivyo basi nikuelekeze meneja wa RUWASA mkoa mtafute huyu mkandarasi na ifikapo jumatatu aweamesharipoti kwa mkuu wa wilaya ya kahama”,amesema.

“Tunamtaka arudishe fedha za malipo ya awali alizokuwa amepatiwa ambazo ni shiringi miloni 186 na mkataba wa kufunja mkataba na huyu mkandarasi uanze haraka sana, mkoa wa Shinyanga unawakandarasi wengi sana kutoka KASHWASA, RUWASA na SHUWASA, wakutane kamatimu ya sekta ya maji ili mradi huu utekelezwe kutumia Force Account kwasabab fedha zipo na wananchi wanataka maji ili ifikapo mwenzi Octoba mradi huu uweumekwisha kamilika”, ameongeza Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Meneja wa RUWAS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela alikili kumuita mara kadhaa mkandarasi huyo kwaajili ya mazungumzo lakini bado imeshindikana mradi huo kukamilika.

“Baada ya kuona kusuasua kwa ujenzi wamradi huu tulijaribu kumuita na kuzungumza naye ili tujue shida ni nini, na tulifanikiwa kutatua baadhi ya changamoto alizozisema lakini bado hali ya utekelezaji haikuwa nzur, Mradi huo wa tanki la maji ulitarajia kuhudumia wakazi wapatao 14,000 waishio vijiji vitatu ambavyo ni Mwaningi, Bulige na Mwazimba lakini mpaka sasa ujenzi wa mradi huo umesumama ”,alisema Mhandisi Payovela.

Nao baadhi ya wakazi wa wakazi wa Buligi akiwemo Malita Chales na Modesta Masai walisema wamekuwa wakikabiliwa na adha ya maji kwa kipindi kirefu na kulazimika kutumia maji ya kwenye bwawa ambalo hutumia kwaajili ya kunyweshea mifugo.

“Hali ni mbaya maji tunayafuata bwawani ambayo ambayo yanatelemka kutoka mlimani, kwenye kipindi hiki cha kiangazi tunaangaika sana, tulijaribu kuchimba visima lakini hatukapata maji, magonjwa nayo ni mengi, tunaiomba serikali ituletee maji safi na salama ili tuache kutumia maji ya bwawa”, amesema Modesta Masai.
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja akikagua utekelezaji wa miradi wa kijiji cha Mwaningi.
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akizungumza.
Mkazi wa Kijiji cha Buligi Malita Chales akizungumza.
Bwawa la Mwaningi linalotumiwa na wakazi wa Buligi.
Bwawa la Mwaningi linalotumiwa na wakazi wa Buligi.
Mradi wa tanki uliotelekezwa na mkandarasi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post