MTANDAO WA BAJETI ZENYE MRENGO WA KIJINSIA MKOA WA SHINYANGA WAKUTANA KUJADILI BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2023/2024


Mratibu mtandao wa bajeti za mrengo wa kijinsia Shinyanga Charles Deogratius akizungumza wakati wa kikao hicho

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mtandao wa Bajeti zenye mrengo wa kijinsia Mkoa wa Shinyanga (SGRBN) umeendesha kikao chenye ajenda ya kufanya tathmini ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 iliyopitishwa na Bunge kwa lengo la kutathmini na kuangalia vipaumbele kwenye bajeti hiyo kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga.

Kikao hicho cha majadiliano kimefanyika leo Jumatano Julai 5,2023 kwenye ukumbi wa jengo la NSSF uliopo Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga kilichoketi kufanya uchambuzi wa bajeti hiyo kwenye sekta nne ikiwemo Kilimo, Elimu, Afya na Maji.

Akizungumza wakati ufunguzi wa majadiliano hayo yaliyowakutanisha mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na vituo vya maarifa na taaarifa chini ya mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP) Mratibu mtandao wa bajeti za mrengo wa kijinsia Shinyanga Charles Deogratius amesema  lengo kuu la majadiliano hayo ni kufanya tathimini ya bajeti iliyosomwa na waziri wa fedha inavipaumbele gani kwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.

“Lengo kubwa la mkutano huu ni kufanya tathmini na majadiliano kulingana na bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 iliyosomwa bungeni je italeta manufaa kulingana na uhitaji uliopo kwenye mkoa huu wa Shinyanga kupitia sekta muhimu nne ambazo ni Elimu, Afya, Kilimo na Maji kwa kuziangazia wilaya zote zilizopo ndani ya mkoa huu”,amesema

“Baada sasa ya majadiliano haya endapo tutabaini kuwa bajeti hiyo hailingani na uhitaji wa eneo husika sisi kama Mtandao wa bajeti zenye mrengo wa kijinsia Mkoa wa Shinyanga tutakwenda kuishauri serikali kupitia viongozi na wawakilishi wa wananchi waweze kufahamu yale tulioyabaini kwenye bajeti hiyo na kuwasaidia waweze kufanya mabadiliko, kuchechemua na kutoa kipaumbele kwenye bajeti mpya inayofuata ya 2024/2025”, ameongeza Charles Deogratius.
Mratibu mtandao wa bajeti za mrengo wa kijinsia Shinyanga Charles Deogratius akizungumza wakati wa kikao hicho
Katibu wa vituo vya Taarifa na Maarifa chini ya TGNP kata ya Ukenyenge Wilayani Kishapu Peter Nestory (KULIA) akizungumza wakati wa majadiliano.
Mkurugenzi wa GAET Member Catherine Kalinga akisoma Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 iliyopitishwa na Bunge wakati wa majadiliano ya kikao hicho.
Mkurugenzi wa Shirika la Children with Disabilitiy Development programme (CHIDEP) Mathias Chidama akizungumza wakati wa majadiliano hayo.
Program Manager Shirika la Green Community Initiatives (GCI) Ngolelwa Masanja akizungumza wakati wa majadiliano hayo.
Mkurugenzi wa Shirika la Childdren with disabilitiy development programme (CHIDEP) Mathias Chidama (KULIA) akiwa na Project Officer kutoka Shirika la Right to Life Mary Charles wakati wa majadiliano hayo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post