ANASWA AKIFANYA MAPENZI KANISANI NA MWANAMKE ALIYEPEWA TALAKA, WAUMINI WAFANYA MAAMUZI MAGUMU

Waumini wa Kanisa la Bunyonga, kaunti ndogo ya Kayonza wilaya Kayunga nchini Uganda ambapo mwanaume na mwanamke walikutwa wakifanya mapenzi katika madhabahu ya kanisa hilo, wamefanya ibada kanisani humo kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa maombi ya utakaso.

Jumanne Julai 5, 2023, saa 2 usiku, mwanaume huyo (23), anayedaiwa kuwa mwanandoa na baba wa watoto wawili, alifumwa na mwanamke ambaye alitalakiwa na mumewe siku chache zilizopita na kulazimika kuishi kwa bibi yake katika kijiji hicho, ambapo kufuatia tukio hilo, Kundi la waumini wa Kanisa la Bungonya lililoko wilayani Kayunga nchini Uganda lilisusia shughuli za ibada.

Waumini katika kanisa hilo waliapa kutofanya ibada kanisani hapo mpaka pale litakapotakaswa baada ya mwanaume mmoja kukutwa akifanya mapenzi na mwanamke katika kanisa hilo Jumatano iliyopita.

Kiongozi wa Kanisa hilo, Aaron Komugisha, amesema timu ya makasisi na waumini wengine kutoka Kitimbwa wakiongozwa na Kiongozi, Dan Kisitu walifanya maombi maalum katika kanisa hilo ili kulitakasa.


Wapenzi hao ambao mwanaume ni mwanandoa mwenye watoto wawili huku mwanamke akiwa ni mtalakiwa walifikishwa kwa Mwenyekiti wa kijiji, George Kanda baada ya kukamatwa wakifanya tendo hilo ambapo aliwaandikia kesi.

“Tumerejesha ibada katika kanisa letu baada ya kuwa na siku ya kufunga na kufanya maombi. Sasa kanisa letu liko safi dhidi ya tendo lile la Kishetani ambalo lilifanyika,” alisema Komugisha.


Kiongozi msaidizi katika kanisa hilo, Esther Nakamate alisema,“tunaomba radhi kwa kila mtu. Tunawataka waje kanisani hapa na kuomba msamaha kwa kile walichokifanya na wasipofanya hivyo hatuwasamehe.”

Tukio hilo la kushtusha, liliibuliwa na mke wa ndoa wa mwanaume huyo ambaye baada ya kumkuta mumewe akifanya mapenzi ndani ya kanisa alipiga kelele iliyowafanya waumini kujaa na kuwakamata watu hao wakiwa utupu.


Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda, tukio hilo lilifanya viongozi wa kanisa hilo kuingia katika mfungo na maombi yasiyokuwa na ukomo ili kukemea kitendo hicho walichokitaja kama "Dhambi ya kushtusha".

Mwenyekiti wa Mtaa wa Bungonya lilipotokea tukio hilo, George William Kanda amesema watu hao waliingia kanisani kupitia dirishani kabla ya kuanza kufanya tukio hilo.

"Waliingia kanisani kupitia dirishani kwa sababu mlango ulikuwa umefungwa," amesema.

"Mke wa ndoa wa mwanaume huyo alipowafumania alipiga kelele, watu wakajaa kanisani na kuwakamata kisha kuwaleta ofisini kwangu. Mtandio wa kichwani na fulana (t-shirt) ya mwanaume vimehifadhiwa kwa mwenyekiti kama udhibitisho," amesema Kanda.

Kanda aliongeza kuwa baada kufikishwa walihojiwa kisha kuachiwa, huku kesi hiyo ikitarajiwa kuendelea kusikilizwa.

Ofisa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai katika Wilaya ya Kayunga nchini humo, Beatrice Ajwang pamoja na kukiri kusikia tukio hilo, amesema hakuna kesi iliyowasilishwa ofisini kwake.

"Viongozi waliotembelea kanisa hili walishtushwa na kitendo hicho," amesema Aaron.

"Watu hao wanatakiwa kutubu dhambi zao mbele ya Mungu," amenukuliwa mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.

Kijiji cha Bugonya kipo takribani Kilometa 35 kutoka mjini Kayunga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post