Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Gift Msuya,akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilayani humo uliofanyika leo Julai 14,2023 Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Meneja Urasimishaji ardhi ya vijiji kupitia mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) Bw. Joseph Osana ,akizungumza wakati wa mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilayani humo uliofanyika leo Julai 14,2023 Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe.Gift Msuya (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilayani humo uliofanyika leo Julai 14,2023 Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mtaalamu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw.Daniel Masunga,akizungumza wakati wa mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilayani humo uliofanyika leo Julai 14,2023 Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Afisa Wilaya ya Chamwino Enock Mligo ,akitoa taarifa wakati wa mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilayani humo uliofanyika leo Julai 14,2023 Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi idara ya uendelezaji vijiji na miji TAMISEMI Bi.Rachel kaduna ,akichagia mada wakati wa mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilayani humo uliofanyika leo Julai 14,2023 Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Diwani kata ya Majeleko Mussa Omary, akichagia wakati wa mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilayani humo uliofanyika leo Julai 14,2023 Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Na.Alex Sonna- DODOMA
WIZARA ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) inakusudia kupanga, kupima na kusajili hati za hakimilki za kimila 500,000 katika halmashauri sita nchini.
Hayo yamesemwa leo Julai 14,2023 na Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe.Gift Msuya, wakati akifungua mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilayani Chamwino.
Mhe.Msuya amesema kuwa Wizara ya Ardhi, kupitia mradi huo iliichagua Chamwino kuwa miongoni mwa wilaya sita ambazo ni Mufindi, Songwe, Mbinga, Maswa na Longido.
“Mradi huu kwa wilaya hizi sita umelenga kuboresha usalama wa milki za ardhi kwa kupanga, kupima na kusajili hati za hakimilki za kimila 500,000 ambapo wilaya ya Chamwino inakusudiwa kunufaika na mradi huu kwa kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi ya wilaya kwa vijiji 60.
“Mradi huu umeanza kutekelezwa na halmashauri yetu na ndio maana leo tumekutana hapa ili kujadili rasimu na hatimaye tuweze kuipitisha rasimu hii na kuwa Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Wilaya ya Chamwino,”amesema Mhe.Msuya
Hata hivyo Mhe Msuya amewataka wadau pamoja na wananchi kushiriki vyema katika utekelezaji wa mpango wa matumizi ya ardhi kupitia mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi
“Nawaomba mchukue mradi huu kama fursa kwenu na kutoa ushirikiano thabiti ili kufanikisha utekelezaji wake na kutatua changamoto hizi Maeneo mengi yalitamani kupata fursa kama hii lakini kutokana na uchache wa rasilimali hawakufanikiwa kufikiwa na mradi”ameeleza Mhe. Msuya
Kwa upande wake Meneja Urasimishaji ardhi ya vijiji kupitia mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) Bw. Joseph Osana amesema kuwa mradi umelenga kuboresha usalama wa milki za ardhi kwa kupanga, kupima na kusajili milki za ardhi zipatazo milioni 2.5
''Ambazo zinazojumuisha hati milki 1,000,000 na leseni za makazi 1,000,000 katika maeneo ya mijini na hati za hakimilki za kimila 500,000 vijijini.''amesema Bw.Osana
Naye Mmoja wa wanufaika wa mradai huo Mwenyekiti wa kijiji cha Ng’ambaku Juma Muyeya, amesema kuwa anaishukuru serikali kwa mradai huo kwakuwa umesaidia kumaliza mgogoro baina ya kijiji chake na kijiji jirani cha Chiboli uliodumu kwa Zaidi ya mika 40.
Social Plugin