Katika hali ya kushangaza, mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Rogan, ameanguka kutoka ghorofa ya tatu hadi ya pili katika Hoteli ya Cate iliyopo eneo la Kitungwa barabara ya Morogoro - Dar es Salaam, baada ya kupitia dirishani, huku akidhani ni mlango wa kuingia chooni.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Mkaguzi Emmanuel Ochieng, amethibitisha kwa kusema: "Tukio hilo limetokea leo alfajili na kwamba askari wa jeshi hilo walifika na kumuokoa mtu huyo ambaye alikuwa amekwama ghorofa ya pili."
Kamanda Ochieng amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wahusika wa hotel hiyo, ilibainika kuwa mtu huyo alifika hotelini hapo jana akiwa na mke wake na walichukua chumba baadaye waliondoka na kurejea usiku.
Kwa mujibu wa kaimu bosi huyo wa jeshi hilo Mkoa wa Morogoro, ilipofika saa 11 alfajiri mke alihisi mume wake hayupo hivyo alianza kumtafuta chooni na baadaye aliona dirisha liko wazi, huku mume wake akiwa ananing'inia.
Social Plugin