Na Mwandishi Wetu, Mbeya
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe jijini Mbeya, tayari kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyikaUwanja wa Luanda jijini humo.
Chongolo akiwa uwanja wa ndege amelakiwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wa mikoa jirani pamoja na Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini.
Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine Chongolo ataelezea hatua kwa hatua usahihi wa makubaliano ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, lengo likiwa kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma kwa viwango vya hali ya juu tofauti na ilivyo sasa.
Kwa mujibu wa ratiba ,mkutano huo utahudhuriwa pia na baadhi ya wananchi kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa.
Social Plugin