*********
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
DIRA ya Maendeleo ya Taifa 2025 imeweza kuzingatia masuala ya kijinsia ambapo mambo mengi yametekelezwa ka kuwapa fursa vijana wa kike na wakiume kujifunza na kuonesha uwezo wao kwenye masula ya kijamii na kiuchumi.
Akizungumza katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) Mtandao wa Jinisia Tanzania TGNP, Afisa Programu Sera TGNP, Bi.Leogate Leokake amesema kwenye Dira hiyo mambo mengi yametekelezwa ikiwemo mradi wa Kujenga Kesho Iliyobora ambapo Mradi huo umewapa fursa vijana kujifunza.
Aidha amesema kuwa Katika Dira ya Maendeleo tumeona shughuli zingine za nchi ikiwemo mikopo ya asilimia 10 pamoja na kushuhudia watoto wa kike kupata ujauzito kurudi shuleni ambapo ni hatua kubwa Dira hiyo imeweza kuzingatia masula ya kijinsia.
Social Plugin