Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida ameongoza ujumbe wa Serikali ya Tanzania kushiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Biashara na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi ya Marekani.
Mkutano huo umefanyika Julai 18, 2023 nchini Kenya ambapo Dkt. Kida amemwakilisha Waziri wa Ofisi hiyo Prof. Kitila Mkumbo ambapo Marekani na Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara na kuvutia uwekezaji.
Aidha, wamejadiliana kutumia kikamilifu fursa za soko la mpango wa AGOA nchini Marekani, Mkataba wa eneo huru la biashara Afrika (AfCFTA) na mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wengine waliohudhuria mkutano huo ni Mwakilishi wa Biashara wa Serikali ya Marekani Mhe. Balozi Katherine Tai, Mawaziri wa Biashara na Uwekezaji wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na sekta binafsi ya Tanzania imewakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Raphael Maganga.
Social Plugin