Na Dotto Kwilasa,DODOMA
Serikali imesema itaendeleza azma yake ya kutoa maji kutoka ziwa Victoria mkoani Mwanza na kuyapeleka Dodoma ili kukabili upungufu uliopo sasa na kukomesha mgao uliopo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph, alisema hayo Jana jiji hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majuku ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2023/24.
Amesema mpango wa serikali kuyatoa maji katika ziwa hilo hajabadilika kwakua Moja kati ya mikakatinya Kitaifa kukabiliaana na tatizo la shida maji mara baada ya serikali kuhamia DODOMA.
"Mipango ya muda mrefu kukabiliaana na hali hii ya shida ya Maji katika mkoa wa Dodoma ni pamoja na kuleta maji ya ziwa Victoria mkoani Mwanza kuja kutatua kero hii ya ongezeko la mahitaji ya Maji ambapo kiasi Cha shillingi Trioni 1.2 zinahitajika Kwa ajili ya mifumo ya kusafirisha maji "amesema
Amesema mpango mwingine WA muda mrefu ni pamoja na ujenzi wa bwawa la Farkwa wilayni Chemba ambapo zaidi ya Sh.biliomi 300 zinatarajiwa kutumika.
Akizungumza kuhusu hali ya upatikani maji katika jiji la Dodoma amesema mahitaji kwa siku ni Lita Milioni 133.4 ambapo uwezo wa uzalisajji ni lita Milioni 68.8.
"Uzalisahji WA maji hivi Sasa katika jiji letu ni Asilimia 50 ya mahitaji hivyo upungufu uliopo ni Lita MILIONI 64 Kwa sasa hali ambayo inatulazimu kutoa huduma zetu Kwa mgao WA masaa 13 Kila siku"amesema
Amesema ili kukabiliana hali hiyo hivi Sasa wanaendelea na mikakatinmbalimbali ikiwemo uchimbaji wa visima katika maeneo mbalimbali ya jiji la dodoma ikiwemo eneo la Nzuguni.
Hata hivyo amesema mikakati mingine ni kuanzia ujenzi wa miundombi ya huduma ya maji taka ikiwemo ujenzi wa mabwa pamoja na mifumo.
Social Plugin