Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MABADILIKO YA TEKNOLOJIA CHANZO CHA KUPUNGUA IDADI ZA SIMU ZA KIMATAIFA ZINAZOINGIA NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Bakari akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika mkutano na Waandishi wa Habari leo Julai 18, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.

  Na  Dotto Kwilasa,Dodoma

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)kupitia Mfumo wake wa Usimamizi wa simu za ndani na kimataifa imebaini idadi ya dakika za simu za kimataifa zinazoingia nchini kupungua kutoka dakika 3,136,692 mwezi Julai 2022 hadi kufikia 2,900,165 mwezi Juni 2023 sawa na asilimia 7.54.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk.Jabir K Bakari ameeleza hayo leo Julai 18,2023 wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Mamlaka hiyo jijini Dodoma na kueleza kuwa idadi ya dakika za simu za kimataifa zinazotoka nchini zimepungua kutoka dakika 2,405,522mwezi Julai 2022 hadi Kufikia dakika 2,226,071mwezi Juni 2023 sawa na asilimia 7.46.

Amefafanua kuwa kupungua kwa simu za kimataifa kunasababishwa na mabadiliko  ya teknolojia na upatikanaji wa chaguzi mbadala za kupiga simu kupitia mitandao ya intaneti kama vile Whatsapp, Facebook, Telegram, Zoom na kadhalika.

"Idadi ya dakika za simu za kitaifa ndani ya mtandao mmoja (onnet) zimeongezeka kutoka dakika 6,172,696,579 mwezi Julai 2022 hadi dakika 7,012,574,045 mwezi Juni 2023 ambayo ni sawa na 13.61% hivyo hivyo idadi ya dakika za simu za kitaifa nje ya mtandao mmoja (offnet) zimeongezeka kutoka dakika4,879,102,325 mwezi Julai 2022 hadi kufikia dakika 5,064,800,480 kufikia mwezi Juni 2023 sawa 3.81%,"amesema 

Amesema ongezeko la simu za kitaifa linasababishwa na ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchini na kwamba katika Kubaini simu za ulaghai TCRA imeendelea kubaini simu za ulaghai zinazoingia hapa nchini na hatua stahiki zimekuwa zikichukuliwa.

" Kutokana na hatua hiyo, idadi ya simu za udanganyifu imeendelea kupunguakuanzia mwaka 2020 hadi Juni 2023, tulibaini matukio machache ya simu za ulaghai yalitokea,katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 mpaka Juni 2023, TCRA imeendelea kuwasimamia watoa huduma za mawasiliano kwa kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa masharti ya leseni zao pamoja na kuzingatia viwango vya ubora ,"amesema.

Dk. Bakari pia amesema, TCRA imefanya maboresho makubwa ya mifumo ya udhibiti wa Sekta ambapo kwa sasa wamejenga uwezo wakufuatilia ubora wa huduma tukiwa ofisini,ili kuhahikisha watoa huduma za mawasiliano ya simu na intaneti, utangazaji (Radio na Televisheni) na posta wanatoa huduma kwa ufanisi na kwa kuzingatia ubora.

"Aidha, TCRA ilifanya ufuatiliaji na kuhakikisha utekelezaji wa masharti ya kanuni na sheria katika maeneo ya ukaguzi wa watoa huduma kwa kukaguzi  watoa huduma 671wa simu na intaneti, utangazaji na postaili kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa sheria, kanuni, miongozo na masharti ya leseni,"amefafanua


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com