Na Mariam Kagenda _ Kagera
Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Jason Rweikiza amewataka wananchi kujiandaa kwa ajili ya kuchangamkia bima ya afya kwa wote itakapoanza.
Dkt Rweikiza ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Buhendangabo baada ya diwani wa kata hiyo Teophily Elieza kutoa kero kwa mbunge kwa niaba ya wananchi.
Amesema kuwa bima ya afya inasaidia pale unapoumwa wakati hauna pesa ya matibabu kwani itakuwezesha kupata matibabu
Katika hatua nyingine amewasisitiza wananchi kuendelea kuchangamkia mbolea ya Ruzuku ambayo serikali ilichangia fedha ili wakulima waipate kwa bei nafuuu.
Kuhusu ujenzi wa jengo la mama na mtoto (Kliniki) Rushaka Dkt Rweikiza amebainisha kuwa atawaongezea mchango wa shilingi milioni tano ambapo mapema mwaka huu alitoa mchango wake ili ujenzi uweze kuanza.
Amesisitiza kuwa daraja la Mishambwa ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 90 likikamilika ,Barabara yake itajengwa na TARURA kutoka Kashozi hadi Rushaka ili wananchi waweze kupita kwa urahisi.
Aidha amechangia shilingi laki nne kwa shule ya sekondari Kalema na shilingi laki tatu kwa shule ya msingi Rushaka B kwa ajiili ya lishe ya wananfunzi shuleni na mipira miwili kila shule huku akitoa mipira kwa timu za vijana kwa ajili ya kujiandaa na ligi ya Rweikiza Cup 2023