Na Mathias Canal - Moshi Kilimanjaro
Mbunge wa Viti maalumu Mhe Ummy Nderiananga ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)amenunua kadi 3500 kwa kwaajili ya Wanachama Wapya wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Kilimanjaro ili kuimarisha chama hicho katika ngazi ya Wanawake
Akizungumza leo Julai 21,2023 mbele ya Vikundi vya Wakinamama Wilaya ya Moshi Vijijini katika ofisi za CCM Wilaya ya hapo amesakuwa amechukua hatua hiyo baada ya maombi ya Wakina mama waliyoyatoa wakati wa ziara zilizofanywa na viongozi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro .
“Niwapongeze viongozi Mbalimbali wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa ziara mlizozifanya, lakini katika ziara zile nimeskia wakinamama wakisema wanahitaji kadi za UWT kwahiyo nikapokea ombi hilo na leo nimelifanyia kazi nimeleta kadi” amekaririwa Mhe. Ummy
Amesema kuwa amenunua kadi 3500 kwa ajili ya Wanachama Wapya wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha hicho na anategemea kila Wilaya katika Mkoa huo itapata kadi 500
Kadhalika Nderiananga ameunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuviwezesha vikundi vya wanawake kutumia nishati safi ya kupikia kwa kutoa Mitungi ya gesi huku akisisitiza umuhimu wa nishati hiyo mbadala.
Mhe Nderiananga amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan imelenga kuhakikisha inapunguza matumizi ya kuni, mkaa na mabaki ya mazao ili kulinda afya za wananchi.
Amesema kuwa licha ya athari za kimazingira zinazotokana na ukataji wa miti unaofanywa na Wananchi Matumizi ya nishati chafu yamekuwa na athari zaidi za kiafya kama takwimu za Athari ya Matumizi hayo zilivyotolewa na Wizara ya Nishati.
Social Plugin