MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wa pili kutoka kushoto akizungumza wakati ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kukagua vyanzo vya maji na kuona upanuzi wa eneo Mowe ambalo maji yanasafirishwa kwa ajili ya matumizi katika Mkoa na Jiji la Tanga kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey HillyMkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kulia akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wakati wa ziara yake wa pili kushoto katika ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema na wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Goefrey Hilly kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wa kwanza kushoto wakati wa ziara hiyo katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza mara baada ya ziara hiyo
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa ziara hiyoMKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akimueleza jambo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara yake kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba aliyesimama katikati wakati wa ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kukagua vyanzo vya maji na kuona upanuzi wa eneo Mowe ambalo maji yanasafirishwa kwa ajili ya matumizi katika Mkoa na Jiji la Tanga
Eneo la Mowe ambapo maji husafishwa kabla ya kwenda kwa watumiaji
Na Oscar Assenga, TANGA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amevitaka vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma wanaodaiwa madeni na Tanga Uwasa kulipa madeni hayo haraka kwa sababu itafikia mahala watakatiwa huduma hiyo.
Kindamba aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kukagua vyanzo vya maji na kuona upanuzi wa eneo Mowe ambalo maji yanasafirishwa kwa ajili ya matumizi katika Mkoa na Jiji la Tanga
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba pamoja na kwamba Tanga Uwasa wamekuwa wakishirikiana na vyombo hivyo lazima wahakikishe wanalipa haraka madeni hayo kwa wale ambao ni wadaiwa sugu ambao hawaonyeshi jitihada za kuyalipa.
“Niwapongeze Tanga Uwasa kwa kufanya kazi nzuri ya kutoa huduma lakini nivitake amevitaka vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma wanaodaiwa madeni na Tanga Uwasa kulipa madeni hayo haraka kwa sababu itafikia mahala mtasitishiwa huduma hii”Alisema RC Kindamba.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa namna anavyoendelea kugusa maisha ya wananchi wa kawaida kwa maana ukienda kwenye maji,afya na elimu utamkuta walichokwenda kushuhudia ni kitu kikubwa sana ambapo Tanga Uwasa wameweza kuongeza uwezo wa kusambaza maji kutoka lita Milioni 30,000,000 mpaka lita milioni 45,000,000.
Hata hivyo alisema mpango wa muda ujao na muda wa kati ni kupanua uwezo wa kuzalisha lita milioni 60 na hilo litawezekana kutokana na mipango waliojiwekea watakuja kutangaza kwenye masuala la hati fungani ambazo zitasaidia kupatikana mtaji wa kuweza kupanua zaidi mradi wa maji kwenye mkoa na Jiji la Tanga.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema wanashirikiana vizuri na taasisi za ulinzi na usalama kutoa huduma zao kwani wao wanatoa huduma kwao.
Mhandisi Hilly alisema wakati mwengine kutokana na sababu mbalimbali kuna kukwama kwenye malipo na kwa sasa wanazidai taasisi hizo takribani Bilioni 1.8 wanashuruku wameanza kupunguza kidogo.
“Kama mlisikiliza Bunge mara ya mwisho tulikuwa tunadai Bilioni 2.4 hivyo wamejitahidi kupunguza Milioni 400 karibia 500 hivyo tunaomba wapunguze deni hilo kutokana na deni ni kubwa na linatukwamisha mambo mengi ya utoaji huduma,ununuaji madawa na ulipaji umeme”Alisema Mkurugenzi huyo.
Naye kwa upande wake Mwenyekiit wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema kwamba madeni yamekuwa yakiwasumbua sana hususani vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma.
“Kwa kweli ni wateja wetu wazuri lakini madeni yamekaa muda mrefu na tuliona tukushirikishe ili uweze kutusaidia Mkuu wa Mkoa na uwasaidia wenzetu wanadai wanapodai walipwe ili waweze kutulipa”Alisema Dkt Fungo..
Social Plugin