Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MNARA NA UWANJA WA MASHUJAA JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi wa Mnara na Uwanja wa Mashujaa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023. Viongozi wengine pichani ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda wakishuhudia tukio hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka mchanga kama ishara ya uzinduzi wa Ujenzi wa Mnara na Uwanja wa Mashujaa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mnara na Uwanja wa Mashujaa katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi, Maafisa pamoja na Wananchi kwenye Maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com