MAJESHI AONYA WANA CCM KUACHA KUDHALILISHANA - "ACHENI KUFUATILIANA,FANYENI KAZI KWA MSHIKAMANO"

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini,Ally Majeshi akizungumza wakati wa kikao cha sekretarieti ya Wilaya na kata kilichofanyika leo Julai 17 2023 kwenye Ukumbi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Na Halima Khoya-Malunde 1 Blog.

 Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini,Ally Majeshi amewataka Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuacha kudhalilishana kwa maneno au kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuacha kufuatiliana ili kujenga mshikamano katika kutimiza majukumu yao.

Majeshi ameyasema hayo leo Julai 17 2023 kwenye kikao cha Sekretarieti ya Wilaya na Kata zote kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya Mkoani humo.

"Uongozi una taratibu zake,nani asiyejua kwenye chama hiki wengi wamejiuzulu kwa sababu ya matatizo yanayowaletea misukosuko kwenye uwazi,punguzeni kusema sema,siku jambo likigundulika litakuwa bayana" amesema Majeshi.

Hata hivyo Makatibu wa Umoja Wa Wanawake (UWT) na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kata mbali mbali Wilaya ya Shinyanga Mjini wameaswa kukaimisha nafasi zilizo wazi hasa nafasi ya Katibu hali itakayosaidia kudumisha na kuleta maendeleo katika Jumuiya izo.

Akizungumza kwenye kikao hicho Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga,Naibu Katalambula amesema kuwa nafasi ya Katibu kwenye Chama ni nafasi nyeti kwa sababu hutegemewa kwenye vikao na Ziara tofauti tofauti sambamba na kuwataka Makatibu hao kutumia vyema nafasi hizo kwa kuwa Wataalamu na siyo wanasiasa.

"Katibu ni mfafanuzi wa jambo,na ili uwe mfafanuzi wa jambo ni lazima uwe Mtaalamu,Katibu hutegemewa kwenye vikao,mikutano na ziara za kamati za sekretarieti kwenye utekelezaji wake,ikitokea kiongozi yeyote hayupo inatakiwa akaimu mwingine ili kufanikiwa katika utendaji waa kazi za kila siku" amesema Katalambula.

Hata hivyo Katalambula ametoa agizo kwa Viongozi wa Jumuiya ngazi ya Kata kufikia Jumatatu Julai 24 2023 kuwe na muundo kamili wa Sekretarieti huku akiwataka Viongozi wanawake kuwa mstari wa mbele kufichiana matatizo wawapo katika kazi.

Naye Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga,Sharifa Hassan amesema kuwa ili kuimarisha na kuendeleza chama hicho ni lazima kudumisha umoja,ushirikiano na kupendana viongozi na wanachama kwa ujumla.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini,Naibu Katalambula akizungumza wakati wa kikao cha sekretarieti ya Wilaya na kata kilichofanyika leo Julai 17 2023 kwenye Ukumbi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Shinyanga.
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini,Sharifa Hassan akizungumza wakati wa kikao cha sekretarieti ya Wilaya na kata kilichofanyika leo Julai 17 2023 kwenye Ukumbi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ,Ally Majeshi katikati,Katibu wa UVCCM,Naibu Katalambula kushoto,Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Sharifa Hassan kulia wakiendelea na kikao cha sekretarieti ya Wilaya na kata kilichofanyika leo Julai 17 2023 kwenye Ukumbi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Shinyanga.
Makatibu wa Chama ngazi ya Wilaya na Kata wakiendelea na kikao cha sekretarieti ya Wilaya na kata kilichofanyika leo Julai 17 2023 kwenye Ukumbi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Makatibu wa Chama ngazi ya Wilaya na Kata wakiendelea na kikao cha sekretarieti ya Wilaya na kata kilichofanyika leo Julai 17 2023 kwenye Ukumbi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post