****************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
MTANDAO wa Jinsia Tanzania TGNP, imeendelea kutoa mafunzo kwa Wanavituo vya Taarifa na Maarifa katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo mafunzo hayo yanagusia masuala ya mnyororo wa thamani kwenye shughuli zao.
Akizungumza katika Mafunzo hayo leo Julai 26,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwanachama wa TGNP, Bi.Rehema Mwateba amesema Mafunzo hayo ni ya siku mbili ambapo leo wamejifunza kawadia na siku ya pili mafunzo yatakuwa kwa vitendo zaidi ili wahusika waweze kupata uelewa mkubwa na kufikia matarajio yao.
Amesema kuna umuhimu mkubwa katika vituo vya taarifa na maarifa kukuza mfuko wao kwaajili ya kuendesha shughuli za uanarakati katika kuhakikisha jamii inaondokana na masuala ya ukatili.
"Kupitia Mafunzo haya tunategemea kuona biashara kubwa zinafanyika ambazo zitaweza kuwasaidia kuwaingizia fedha nyingi wanavituo vya taarifa na maarifa kwaajili ya kukuza mfuko wao". Amesema Bi.Mwateba.
Social Plugin